Kamati ya Sheria na Haki za wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara huku ikiwa imepitisha jina la Hassan
Ramadhani ‘Kesi’ kuitumikia Young Africans kuanzia msimu huu 2016/17 baada ya
kuona kuwa hana tatizo katika usajili badala yake madai ambayo pande husika
zinaweza kudaiana wakati mchezaji anaendeleza kipaji chake.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa imepitia usajili
wa timu zote na kujiridhisha kwamba suala la mchezaji Hassan Kessy limeegemea
kwenye madai na si usajili ambako Simba ndiye mdai kwa kumtuhumu mchezaji huyo
kuwa alianza kuitumikia Young Africans kabla ya kumaliza mkataba wake Simba SC.
Mkataba wake ulifika mwisho, Juni 15, 2016.
Kama ni madai Simba inaweza kuendelea kumdai Kessy au Young Africans
wakati mchezaji huyo anatumika uwanjani kwa mwajiri mpya.
TFF inafuatilia na kuangalia haki ya Simba namna ya kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa zamani.
TFF inafuatilia na kuangalia haki ya Simba namna ya kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa zamani.
Kanuni hazimzuii mchezaji kuendelea kucheza kwa hoja ya madai badala yake
suala hilo linaweza kumalizwa wakati mashindano yanaendelea.
Kamati inaendelea
kupitia malalamiko na pingamizi za wachezaji wengine na inatarajiwa kutoa
taarifa rasmi kuhusu wachezaji wote wakati wowote kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment