Saturday, August 27, 2016

MAKONDA AAGIZA VIONGOZI WA DINI WASIPANGE FOLENI KWENYE OFISI ZA SERIKALI, WAHUDUMIWE HARAKA.



Mkuu wa mkoa wa Dar  es Salaam,  Paul Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es Salaam, pamoja  na watendaji wote serikali katika mkoa huo, kuwahudumia viongozi wa dini kwa haraka iwezekanavyo.

Kauli  hiyo  ameitoa wakati  wa kuweka jiwe la msingi  la ofisi ya  BAKWATA  makao makuu, na kusema kuwa si busara viongozi wa dini kuwaacha wakipanga foleni kwenye  ofisi za serikali kwaajili ya kusubiri huduma.

"Natoa wito kwa ma DC wa mkoa wa Dar es Salaam, na watumishi wote serikali ni marufuku kumkuta kiongozi wa dini kumkuta amepanga foleni anapokuja kwenye ofisi yako, nikibahatika kupitakwenye ofisi yako nikamkuta sheikh amepanga foleni, Askofu yupo kwenye foleni, Mchungaji amekaa kwenye foleni wewe ni halali yangu, lazima viongozi hawa wapate heshima  yao, Alisema.

Mkuu huyo wa  mkoa wa Dar es Salaam, ambae ndiye aliyeanzisha wazo la kujenga ofisi ya BAKWATA  makao makuu, alisema  amefikia uamuzi huo  wa kujenga ofisi  ya BAKWATA kutokana  na  namna anavyowathamini  viongozi dini.

Aliongeza kuwa Msimamo Rais Magufuli ni kuwaheshimu viongozi wa dini, na kwamba yeye lazima afuate nyayo za Rais kwa kuwapenda viongozi wa dini.

Aidha, Mkuuhuyo wa mkoa wa Dar es Salaam, ambae alikuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe lamsingi, alitumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa dini katika mkoa wake waendelee  kuhubiri amani na  kuwataka wasiwaruhusu waumini wao kushiriki katika  maandamano ya UKUTA ili kuepuka kujiingiza katika  kuvuruga amani.

Alisema ataendelea kuhakikisha kwamba amani inakuwepo katika mkoa Dar es Salaam na yeyote atakaejaribu kuichezea amani hiyo sheria itamshughulikia.

Awali akizungumza katika hafla  hiyo, Sheikh  mkuu wa  Tanzania, Mufti  Aboubakari Zubeir,alisema waislamu wanamshukuru Mkuu huyo wa mkoa  kwa kuwajengea ofisi BAKWATA kwakuwa  ofisi hiyo itawawezesha kufanya kazi zao kwaufanisi zaidi.

Mufti Zubeir alisema  katika utawala wake  amewka lengo la  kuwaunganisha waislamu kuwa kitu  kimoja  kwakuwa  hiyo ni Amri ya  Mungu na kwamba ataendelea kulisimamia hilo ili kuona waislamu  wote wanashikamana katika kamba moja na wala wasfarakiane.

Ofisi hiyo  inatarajiwa kugharimu shilingi Bilioni tano n a milionimiambili itajengwa chini ya ufadhili wa GSM kupitia usimamizi wa  mkuu wa mkoa wa  Dar es Salaam.                                                                                                                                                                   


No comments:

Post a Comment