Wednesday, August 31, 2016

HALMASHAURI YA BAGAMOYO, YAFANIKIWA KUKUSANYA MAPATO MARA KUMI ZAIDI.

Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy, kushoto, na kulia ni Makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Mohamedi Usinga
.................................

Ukusanyaji mapato ya ndani katika Halmashauri ya  Bagamoyo umeongezeka mara  kumi  zaidi ukilinganisha na siku  za nyuma.
Hayo yamebaishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Halmashauri mara baada ya kumaliza kikao cha baraza la madiwani kilichomalizika  leo.

Mwenyeki huyo wa Halmashauri alisema kuwa Halmashauri ya Bagamoyo imejipanga vizuri katika vyanzo vyake vya mapato ili kukusanya mapoto halisi yanayo  kusudiwa na kufikia lengo lililowekwa na Halmashauri katika  kukusanya  mapato ya  ndani.

Aliongeza kuwa utekelezaji  wa miradi  mbalimbali ya  maendeleo unategemea ukusanyaji mzuri wa mapato ambapo kwa namna walivyojipanga wameweza kukusanya  mapato mara  kumi  zaidi ya kawaida.

Akivitaja vyanzo vya mapato ambavyo  wameweza kuvisimamia vizuri  ni  pamoja na Kituo  cha mabasi, Geti  la kukusanya  ushuru  kwa maliasili  sanzale, Ushuru wa samaki pamoja na machimbo ya  Mchanga yaliyo eneo la Kiromo ambapo hivi karibuni  wanatarajia kupeleka nguvu zaidi kwenye ukusanyaji  kodi zamajengo.

Kufuatia Hali hiyo, Mwenyekiti huyo ambae ni Diwani wa kata ya Fukayosi, alisema ana matumaini makubwa kwamba wanaweza kufikia lengo la kukusanya  bilioni 2 na milioni mia nane ili kukidhi  mahitaji ya Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Aliongeza kuwa, katika mikakati ya kuhakikisha halmashauri inakusanya  mapato ya kutosha, imeongeza kodi za pango kwa watumishi wanaoishi kwenye nyumba za serikali na kwamba tayari watumishi wa serikali wamepewa mikataba mipya kwaajili ya ongezeko la kodi ya   pango.

Aidha, aliongeza kuwa, katika makusanyo hayo asilimia kumi inarudishwa kwenye kata zinazosimamia  makusanyo hayo ili kata nazo  zifanye  maendeleo yake ya kata ambapo hiyo itakuwa ni motisha  kwa kata kuendelea kukusanya mapato  kwa wingi.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa Halmashauri alisema kuwa, licha ya kasi ya ukusanyajiwa  mapato  lakini bado wanaendelea kumthamini mwananchi wa kawaida wa chini anaefanya  biashara ndog ndogo.

Alisema kwa wafanyabiashara ndogondogo ambao hawapo  kwenye fremu hawatalipa kodi kama alivyoagiza Rais wa Jamhuriya  Muungano, vinginevyomtu awe ameweka biashara yake kwenye fremu.

Alitolea mfano wa wauzaji mkaa wa majumbani hawatalipa ushuru  mpaka wawe kwenye fremu na wakaanga chipsi wa mitaani  pia hawatalipa ushuru vinginevyo  awe  anakaangia ndani ya fremu









No comments:

Post a Comment