Friday, August 5, 2016

RC. MAKONDA ATEMBELEA FFU DAR ES SALAAM



Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh. Paul Makonda, amewataka  askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia FFU jijini Dar es salaam kudumisha uzalendo  walionao katika kulinda  usalama wa raia.

Mkuu wa mkoa Makonda  ameyasema hayo wakati alipotendelea kikos hicho leo ambapo aliwasifia  kwa kazi nzuri wanayofanya ya  kujituma.

Makonda aliongezea kwakusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu.

Rc Makonda amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba wafanye dar iwe kama dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta. Rc.Makonda anaamini dar inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa. 

Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt.John Magufuli, ombi la Makonda lilikua juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika bila kuchelewa.

No comments:

Post a Comment