Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman
Mbowe, amesitisha shughuli za maandamano zilizokuwa zimepewa jina la (UKUTA)
kwa Muda wa mwezi mmoja,kwa kile alichodai baada ya kuombwa na viongozi wa Dini
na taasisi Mbalimbali, ambapo maandamano hayo yalitarajiwa kufanyika kesho
Septemba Mosi nchi nzima.
Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha kwa maandamano hayo mapema leo mchana wakati akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara za viongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa kutafuta Suluhu .
Mbowe ametoa kauli hiyo ya kuahirisha kwa maandamano hayo mapema leo mchana wakati akizungumza na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.Amesema sababu kubwa za kuahirisha maandamano hayo ni busara za viongozi wa dini ambao wameiomba Chadema iwape muda wa kutafuta Suluhu .
Viongozi mbalimbali wa
kidini pamoja na Taasisi mbalimbali za kiraia hatimaye wamesaidia kutokomeza
UKUTA kwa kuuomba uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
kuahirisha Oparesheni hiyo iliyopangwa kufanyika Septemba mosi nchi
nzima.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari katika Makao Makuu ya CHADEMA Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,
Freeman Mbowe amesema Viongozi hao wakuu wa kidini wamewaomba na
kuwasihi katika vikao mbalimbali walivyokaa pamoja nao na kusema tunaheshimu
viongozi hao.
Mbowe amesema wanawapa
muda wa wiki mbili au tatu ili waonane na Rais Magufuli kwa lengo la kutafuta
suluhu ya kudumu ya mgogoro huu wa kisiasa na kuliepusha taifa na machafuko ya
kisiasa.
Pia amesema Viongozi wa
Taasisi za kiraia kama vile Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Taasisi
ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Wahariri na Jukwaa la Katiba nao wamewasihi
kuahirisha UKUTA kwa muda ili kutoa fursa kwa jitihada za mazungumzo na
majadiliano kufanyika.
"Sisi CHADEMA
tunatambua na kujali haki zetu za kisiasa kama zilivyofafanuliwa katika Katiba
na Sheria za nchi yetu. Hata hivyo tunajali na kuheshimu kwa kiasi kikubwa
zaidi haki za Watanzania ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya
maisha yao" amesema Mbowe
Amesema wanawaomba
kuwatangazia viongozi weo wa ngazi zote CHADEMA, pamoja na wanchama,wafuasi na
Watanzania wote kuhairisha kwa mwezi mmoja mikutano na maandamano ya amani
yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho Septemba Mosi.
No comments:
Post a Comment