Tuesday, August 30, 2016

WAISLAMU WA BOKO BEACH WAOMBA MSAADA WA KUJENGEWA MSIKITI


Picha ya Msikiti unaotarajiwa kujengwa Boko Beach, kama inavyoonekana kwenye mchoro.
Katibu wa Swaffatul Mukarama,Abdul Saidi Shomari, akielezea kuhusu nama walivyopata wazo la kujenga msikiti katika eneo hilo  la Boko Beach Manispaa ya  Kinondoni jijini Dar  es Salaam. 
Katibu wa Swaffatul Mukarama,Abdul Saidi Shomari, akiwaomba waislamu popote walipo kuchangia ujenzi wa msikiti katika eneo hilo  la Boko Beach Manispaa ya  Kinondoni jijini Dar  es Salaam. 
Mwenyekiti wa Swaffatul Makarama, Yusufu Mjugu akifafanua jambo mbele ya waislamu waliohudhuria kikao hicho
Mwenyekiti wa Swaffatul Makarama, Yusufu Mjugu akitoa mchanganuo  wa  fedha hizo zitakavytu mika kwenye ujenzi wa  msikiti mbele ya waislamu waliohudhuria kikao hicho
Jengo la Msikiti unaotarajiwa kujengwa  kama  linavyoonekana kwenye mchoro
Jengo la Msikiti unaotarajiwa kujengwa  kama  linavyoonekana kwenye mchoro
......................................................................................................................

Waislamu wa maeneo mbalimbali wameombwa  kuchangia ujenzi wa Msikiti  katika mtaa wa Boko beach jijini Dar  es Salaam kutoka  na eneo hilo  kukosekana msikiti kwaajili ya ibada ya swala.

Katika kikao kilichoitishwa na waislamu wa mtaa huo wa Boko Beach   ili kujadili namna ya kujenga  Msikiti, Katibu madrasa ya Swaffatul Mukarama, ambao ndio wasimamizi wa juenzi  huo, Abdul Saidi  alisema wamefikia uamuzi wa kuanzisha wazo  la kujenga msikiti  kwakuwa eneo hilo halina msikiti na kwamba amewaomba waislamu kutoa ushirikiano ili kufanikisha  ujenzi huo.

Alisema eneo hilo halina Msikiti licha ya kuwepo kwa waislamu wengi hali inayopelekea kukosekana swala  ya jamaa, na kuongeza kuwa ili upate swala ya jamaa unalazimika kutembea umbali mrefu mpaka Boko basihaya mahalipo ulipo msikiti.

"Eneo hili lote la Boko Beach halina Msikiti waislamu wa hapa tunaikosa swala ya jamaa na pia watoto wetu wanakosa kujua umuhimu wa swala licha ya kuwa tunawasomesha Madrasa" Alisema katibu Ust. Abdul. 
 
Aliongeza kuwa awali walikuwa hawana hata madrasa ya kusomesha watoto, lakini mama mmoja Bi Zuena Salum alitoa sehemu ya kiwanja chake na kwaajili ya ujenzi wamadrasa ambayo inaendelea mpaka sasa.

Kufuatia uhitaji wa msikiti, waislamu wa eneo hilo pamoja na mama aliyetoa eneo la madrasa kuwa uandaliwe mchoro na lijengwe jengo litakalojumuisha Msikiti  pamoja na Mdrasa ya vijana.

Alisema kufuatia hali wamelazimika kusajili bodi ya wadhamini ili  kusimamia mambo kwa ufanisi bila ya kukiuka sheria za nchi na kwamba usajili upokatika hatua za mwisho  kukamilika.

Akielezea mchakato wa ujenzi huo wa msikiti, Katibu wa bodi ya wadhamini Wanura Maranda, alisema hatua za awali zimeshakamilika ikiwa ni pamoja na kupata michoro ya jengo na makadirio ya gharama ya ujenzi kutoka kwa wakadiriaji majengo.

Aliongeza kuwa, kutokana na  ufinyu wa Kiwanja jengo hilo  litakuwa na ghorofa mbili ili  kupata sehemu ya kuswalia na madrasa ya watoto, aliongeza kwa kusema kuwa walitamani kujenga zaidi ya ghorofa mbili  lakini  hali kifedha wamehofia gharama itakuwa kubwa hali ya  kuwa hawana hata pesa ya kuanzia ujenzi  huo.

 Ust. Maranda alizitaja gharama za ujenzi wa msikiti huo kuwa ni  shilingi milioni mia tano na arubaini na saba, laki moja themanini na nne, mia sita  kumi  na tano tu, 547,184,615/= ili  kukamilisha ujenzi  huo.

Aidha, alisema kuwa wao wameanzisha wazo hilo lakini hawana fedha, hivyo aliwaomba waislamu  popote walipo kutoa ushirikiano na kufanya biashara na MwenyeziMungu kwa kuchangia ujenzi  huo wa msikiti.

Alibainisha kuwa waislamu wanaweza kuchangia kwa njia tofauti, kuchangia kwa kila muislamu alichojaaliwa, mtu mmoja peke yake ikiwa ataweza kujitolea kujenga jengo lote, kwakutoa vifaa au kwa kuingiza fehda katika akaunti iliyofunguliwa Benki ya Amana kwa jina la ya Swaffatul Mukarama, namba ya Akaunti ni 003140405030001 piya una kuwasiliana moja kwa moja na katibu wa Bodi  kwa namba 0713422774 Mwenyekiti namba 0713326287.

Madrasa ya Swaffatul Mukarama imeanzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi 3. kutokana na wazo la Bi Zuena kutoa sehemu ya kiwanj chake ambapo mpaka mpaka sasa ina wanafunzi 70.

No comments:

Post a Comment