Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza kwenye kikao cha
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo, katika kikao chao madiwani
,ambapo kwa kauli moja waliazimia kumuomba Rais kufuta hati miliki ya shamba la
Soap and Allied industries limited ambalo linamilikiwa na Hamidu Balma lililopo
mkoani Pwani kwa kushindwa kuliendeleza.
Madiwani wa kimsikiliza Kwa makini Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega katika kikao cha halmashauri ya wilaya ya
Mkuranga. Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Kwa kauli moja
wamepitisha mazimio ya kuunda kamati itakayokwenda Kwa Waziri Mkuu ili kumuomba
rais afute hati miliki ya shamba namba 271, linalomilikiwa na mwekezaji, Hamidu
Balma.
Shamba hilo ambalo lenye hekari 1750 ambalo
lipo katika kata ya Mwandege limeingia katika mgogoro mkubwa na wananchi wa
kijiji cha kazole, hadi kufikia hatua ya wananchi hao kulala mahabusu Mara
kadhaa kwasababu ya wanakijiji hao kuingia katika shamba hilo ambalo limekaa
zaidi ya miaka 28 bila kuendelezwa. (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
Chanzo, jiachie blog.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, filbarto Sanga akizungumza katika mkutano
wa baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Mkuranga ,ambapo
alisisitiza suala la uimarishaji wa ulinzi na usalama ndani ya wilaya hiyo, kulia
ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Juma Abeid (alie
simama) akizungumza katika kikao hicho cha baraza la madiwani lililofanyika
jana
Diwani wa Kata ya Mwandege Adolph Edward akichangia hoja katika kikao
hicho cha Baraza la madiwani katika Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo ziliibuka
hoja mbalimbali ikiwamo ya mwekezaji Hamidu Balma aliyeshindwa kuendeleza
shamba namba 271, lililopo katika kataka ya Mwandege
No comments:
Post a Comment