Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem
Shabati akijisajili kabla ya kuchangia damu leo katika hospitali hiyo. Kushoto
ni Msajili wa damu, Titus Mhokole.
.............................................................................................
Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem
Shabati amewataka Watanzania kuwa na tabia ya kuchangia damu ili kuokoa maisha
ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Balozi Shabati amefika leo katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili kuchangia damu na kuwahamasisha watu wajitokeze
kwa wingi ili kuchangia damu.
Amesema kila mtu ana wajibu wa kuchangia damu
kwa kuwa ni muhimu kwa maisha ya wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.
Pia, Balozi Shabati amesema lengo la kuchangia
damu ni kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi yake ambao ni wa muda mrefu
na wa kihistoria.
Katika hatua nyingine, Ofisa Uhusiano wa
hospitali hiyo, Neema Mwangomo amesema kwa wastani hospitali hiyo inakusanya
chupa 40 hadi 50 kwa siku, lakini mahitaji kwa siku ni chupa 80 hadi 100.
Amesema makundi makubwa yanayohitaji damu kina
mama wajawazito, watoto wenye saratani, majeruhi wa ajali na wagonjwa
wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji.
Mwangomo amesema mwanaume mwenye umri wa miaka
18 hadi 65 ndiye anapaswa kuchangia damu wakati mwanamke ni miaka 18 hadi 62.
Amesema kigezo cha pili ni mtu anayechangia
damu anapaswa kuwa na uzito wa kilo 50 na kuendelea na kwamba mtu anapaswa kuwa
na wingi wa damu kuanzia asilimia 85.
Mwanamke anaweza kuchangia damu mara tatu kila
baada ya miezi minne wakati mwaume mara nne kila baada ya miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment