Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Mh.
Miraji Jumanne Mtaturu amesema hakuna demokrasia yoyote duniani inayohubiri
wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo hivyo kila mwananchi anapaswa kushirikishwa
katika kuchagua viongozi wake, kukaa na viongozi wake kupanga miradi ya
maendeleo kama vile kuchangia ujenzi wa shule, zahanati, maabara na maendeleo
mengine.
Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo wakati wa
kikao cha kazi kati yake na Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Wenyeviti
wa Vijiji na Watendaji wa Kata na Vijiji katika mafunzo yaliyofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Alisema Ushiriki wa wananchi katika shughuli
za maendeleo kwa kutumia nguvu na akili katika kukamilisha na kumiliki miradi
ya kijamii ni njia mojawapo itakayowafanya wananchi kuwa na uchungu na mali
pamoja na maendeleo katika jamii husika.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya demokrasia katika Wilaya hiyo hususani katika shughuli za kijamii kama vile kuchangia ujenzi wa maabara jambo lililopelekea Wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika ujenzi wa maabara kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo katika Wilaya ya Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya demokrasia katika Wilaya hiyo hususani katika shughuli za kijamii kama vile kuchangia ujenzi wa maabara jambo lililopelekea Wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika ujenzi wa maabara kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo katika Wilaya ya Ikungi.
“Wataalamu wa Sayansi na viongozi mashuhuri wamewahi kusema Demokrasia bila maendeleo sio demokrasia, Hayati Mwalimu julius Kambarage Nyerere na Profesa Issa Shivji waliwahi kuandika kuwa demokrasia ya kweli ni ile inayowasaidia wananchi kutoka katika hali moja kwenda kwenye hali nyingine ambayo ni bora zaidi kuliko ile waliyo nayo, hivyo tukiongelea kuwashirikisha wananchi katika mipango na mikakati ya kuondokana na umasiki na si vinginevyo” Alisema Mtaturu
Dc Mtaturu alisema kuwa mwenyekiti wa Kijiji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), CHADEMA, ACT WAZALENDO, CUF au chama chochote hapaswi kuongoza wananchi kwa matakwa yake binafsi bali ni lazima kufuata taratibu, kanuni, sheria na taratibu zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yao.
Aliwaelekeza wenyeviti wa Vijiji kuwa majukumu yao ni kuongoza vikao vya Halmashauri ya Kijiji na kuongoza mkutano mkuu wa Kijiji sio kuuza ardhi ya kijiji kiholela, Kumnyang’anya mtu ardhi au kupiga faini yoyote wanayojisikia na ndio maana kunakuwa na watendaji wa Vijiji ambao ni wataalamu hivyo wana majukumu muhimu katika kuwashauri wenyeviti wa Vijiji.
Dc Mtaturu pia amewataka viongozi hao kutambua kuwa uchaguzi ulimalizika Octoba mwaka jana na chama kilichoshika dola ni Chama Cha Mapinduzi(CCM) hivyo kutokana na uchaguzi huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipewa ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 hivyo ilani inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kwa vile kila kiongozi wa Kijiji yupo ndani ya serikali anapaswa kutelekeza ilani ya CCM kwani huo ni utaratibu wa vyama vinavyoshinda popote dunia.
Baadhi ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, na baadhi ya watendaji wa Vijiji Wilayani Ikungi hawajawahi kupatiwa mafunzo ya muongozo wa kiutendaji hali iliyopelekea baadhi yao kutotimiza wajibu wao na wengine kufanya kazi nje ya mipaka yao.
“ Kupitia kikao/mafunzo haya Uonevu wowote, kosa lolote, matumizi mabaya ya madaraka yatakayofanywa aidha na Mtendaji wa Kata,Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji sitalifumbia macho nitakuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni, tulizowekeana kama serikali” Alisema Mtaturu
Sambama na hayo Dc Mtaturu aliwasihi viongozi hao kuwaunga mkono askari polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwani bila usalama na amani katika jamii inayotuzunguka hakuwezi kuwa na maendeleo.
No comments:
Post a Comment