Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Hemed Mwanga, anawatangazia wananchi wote
wa Bagamoyo kuwa, kesho siku ya jumamosi Tarehe 27-08-2016 kutakuwa na zoezi la usafi wa mazingira
litakalo anza saa 12 asubuhi mpaka saa 3 asubuhi.
Hivyo
basi kila mwananchi anapaswa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira na
kwamba biashara zote haziruhusiwi kufunguliwa mpakazoezi la usafi litakapokwisha.
Aidha,
baada ya kufanya usaf, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Majengo ambapo
atawahutubia wananchi.
Katika
Mkutano huo wadao na Taasisi mbalimbali
zitakuwepo wakiwemo DAWASCO.
Wananchi wote mnatakiwa kushiriki usafi na kuhudhuria
mkutano ili kumsikiliza mkuu wa wilaya.
Imetolewa
na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
Tarehe 26-08-2016
No comments:
Post a Comment