Mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, kulia akimkabidhi madawati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mh. Saidi Zikatimu kushoto
Mbunge wa
viti maalum mkoa wa Pwani Mh. Subira Mgalu
leo amekabidhi madawati 20 kwa
Halmashauri ya Chalinze ikiwa ni katika kuunga mkono kampeni ya Mh. Rais wa
Jamhuri ya muungano kuhusu utengenezaji wa Madawati ya shule kwa nchi nzima.
Mh. Mgalu alisema ameamua kutoa madawati hayo ili kuunga mkono juhudi
za Rais ambapo kutokana na kuguswa ameamua kutoa msehemu ya Mshahara wake ili kuchangia Madawati.
Akipokea Madawati hayo, Mwenyekiti wa halmashauri
ya Chalinze, Saidi Zikatimu, amemshukuru Mbunge huyo kwa mchango huo wa
madawati na kumuagiza Afisa elimu msingi kuhakikisha madawati hayo yanafika
kwenye shule yenye mahitaji huku akisisitiza kuyatunza.
Mh. Zikatimu alisema kufuatia wito wa Rais
Magufuli katika utengenezaji wa madawai
madiwani wa Halmashauri ya Chalinze pamoja wataalamu wao wameweza kuchangia kwa
namna moja au nyingine katika upatikanaji wa madawati katika halmashauri hiyo mpya ya Chalinze
iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, kulia akizungumza mara baada ya kukabidhi madawati katika ofisi za Halmashauri ya Chalinze, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa, na wa pili kushoto niMwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mh. Saidi Zikatimu, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa madawati hayo na Mbunge wa viti maalum mkoa wa pwani, Subira Mgalu.
Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wakijaribu kukalia madawati hayo.
No comments:
Post a Comment