Mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu
Mwandamizi wa Polisi, SSP- Adama Amani
Maro, akizungumza katika uwanja wa shule ya
msingi majengo mjini Bagamoyo.
........................................................................................................................................
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya
Bagamoyo, Majid Mwanga amewataka
wananchi kuacha kujiingiza kwenye maandamano yaliyoandaliwa siku ya tarehe
moja mwezi wa tisa kwakuwa maandamano hayo yameshapigwa
marufuku na kwamba yeyote atakaeandamana siku hiyo atakuwa amekiuka sheria za
jamhuri ya Muungano na atachukuliwa hatua.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya amb ae pia ni mkuu wa wilaya, aliyasema hayo
alipokuwa akizungumza na wananchikatika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo mjini Bagamoyo.
Alisema katika
wilaya yake hapendi kumuona mtu
akivunja sheria na
kwamba yeyote aliyejiandaa kuvunja
sheria atafute wilaynyingine na sio Bagamoyo.
Alisema kuna watu wanapita na kuwashawishi
wananchi waandamane siku ya tarehe moja Septemba, nataka niwahakikishie
hatutamuacha mtu avuruge amani katika
wilaya ya Bagamoyo na atakaechezea mamlaka
tutamuonyesha. Alisema.
Kwa upande wake mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu mwandamizi wa
Polisi, SSP-Adam Maro alisema polisi kwaajili ya usalama wa raia na
mali zao na kwamba yeyote atakaebainika anataka kuvuruga usalam wa raia na mali zao, polisi itamshughulikia.
Aliongeza
kuwa, atakaeandamana siku ya
tarehe moja septemba
anatafuta ubaya na polisi kwakuwa
polisiitasimama katika kutekeleza
wajibu wake.
Aidha, aliyataka mashirika ya kimataifa
yanayotetea haki za binadamu kuangalia vyanzo vya uvunjifu wa amani kabla ya kutetea haki za binadamu,
ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea
badala ya kusubiri madhara yatokee ili mashirika hayo yatoe lawama.
Alisema kitu kilichozuiliwa kisheria kikifanyika kwa
nguvu ni kuvunja sheria, "inakuaje anaesimamia sheria ya nchi isivunjwe
anaambiwa amevunja haki za binadamu"? Alihoji, SSP- Maro na kuongeza kuwa ifike wakati sasamashirika
ya kimataifa yanayotetea haki za
binadamu yatoe elimu kwa jamii juu ya utiii wa sheria bila shuruti ili raia
waelewe mipaka yao na serikali itimize
wajibu wake wa kuwatumikia wananchi.
Alisema jeshi la polisi wilayani Bagamoyo litaendelea kutimiza wajibu wake wa
kulinda usalama wa raia na mali zao
hivyo amewataka wananchi kutoa
ushirikiano ili kufanikisha kazi za polisi
na hatimae kuishi pamoja kati
ya polisi na raia
bila ya uadui.
"Polisi
peke yao hawawezi kulinda amani bila ya raia wema kutoa ushirikiano na huu ndio
ushirikiano tunaoutaka", Alismea,
OCD, SSP-Maro.
Aidha, mkuu huyo wa
Polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu Mwandamizi waPolisi, SSP- Adam Maro alisema
watu wa Bagamoyo wanahistoria ya ustaarabu, hivyo wasikubali
kudanganywa kuharibu sifa
yao ya ustaarabu kwa kufanya maandamano
ambayo yamekatazwa kisheria.
No comments:
Post a Comment