Taarifa za awali kutoka eneo la tukio
zinasema kuwa Ng'ombe hao walitolewa katika kijiji cha Makurunge
kata ya Makurunge ambako kulitokea
mapigano kati ya wakulima na wafugaji baada ya wafugaji kuingiza Ng'ombe kwenye
shamba la mkulima na kuharibu mazao.
Akielezea kwa ufupi katika eneola tukio mkuu wa polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi, SSP. Adam Maro alisema mara baada ya kupata taarifa za kuwepo vurugu kati ya wakulima na wafugaji katika
kijiji cha Makurunge, polisi walifika eneo la tukio ili kulinda usalama wa raia
na mali zao.
SSP Maro alisema wafugaji waliingiza Ng'ombe katika shamba
la mkulima na kusababisha mazao kuliwa, hali iliyopelekea wakulima
kuzuia Ng'ombe.
Aliongeza kuwa mara baada ya wakulima kuzuia Ng'ombe
hao ndipo kundi la wafugaji walipoanzisha fujo kwa kuwapiga
wakulima na silaha m,balimbali za jadi.
Alisema polisi walipofika eneo la tukio na kukuta
wafugaji wamekimbia walilazimika
kuondoka na Ng'ombe
mpaka kituoni ikiwa ni njia ya kuwapata wahusika wenye mifugo hiyo ambao
ndio wahusika wa vurugu hizo.
Hata hivyo, polisi waliwaongoza Ng'ombe hao
wakiwa na gari ya polisi iliyokuwa imewasha taa za kuongozea msafara ambapo walipofika eneo la Ukuni Bagamoyo mjini maarufu kama
barabara mpya, Gari aina Fuso ambalo
namba zake hazikupatika mara moja limegonga msafara huo wa Ng'ombe na
kusababisha vifo vya Ng'ombe watano papo
hapo.
No comments:
Post a Comment