Wednesday, August 24, 2016

BAYPORT YAGAWA HATI ZA VIWANJA

hati 1
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akimkabidhi hati mteja wao Mary Simon, baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinapatikana kwa njia ya fedha taslimu na mikopo maalumu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Kulia ni Meneja Mikopo wa taasisi hiyo, Nasibu Kamanda.
 .....................................................................................


TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana imeendeleza utaratibu wake wa kugawa hati kwa wateja wao walionunua viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa njia ya mikopo na fedha taslimu.

Mradi huo wa Vikuruti ulizinduliwa mwaka jana, ambapo baada ya kufanikiwa kwake, taasisi hiyo ikaanzisha miradi mingine mitano ambayo ni Kigamboni, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha na Kilwa, huku ikiweka utaratibu rahisi na nafuu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, alisema kwamba kugawa hati kwa wateja wao ni mwendelezo wa huduma nzuri zinazotolewa na taasisi yao kwa ajili ya kuwakomboa wananchi katika suala zima la ardhi.

Alisema kwamba makubaliano yao ni kuhakikisha taasisi inasimamia sualaa la hati ili wateja wao wasisumbuke kutokana na mchakato mzima wa utendaji kazi wao unaotoa urahisi juu ya upatikanaji wa viwanja vyao vyenye hati.

“Tunaendelea na kutoa hati kwa wetu walionunua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, ambapo Watanzania wengi walichangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo, ambavyo ukiacha vya Vikuruti, wateja wetu pia wanaweza kukopa fursa hii ya ardhi kwa miradi yetu ya Kimara Ng’ombe (Bagamoyo), Msakasa (Kilwa), Tundi Songani (Kigamboni), Boko Timiza (Kibaha), Kibiki na Mpera (Chalinze) na Kitopeni (Bagamoyo).


Naye mteja wa Bayport aliyopewa hati yake, anayejulikana kwa jina la Mery Simon Anthony aliipongeza Bayport kwa kutoa huduma nzuri kiasi cha kumfanya amiliki kiwanja chenye hati, huku kikiwa hakina mlolongo wowote.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu nimepata hati yangu kwa haraka na sijapata usumbufu wowote, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi katika miradi hii ya viwanja vya Bayport kwa sababu ni rasilimali nzuri,” Alisema.

Naye Sixtus Francis Kilenga alisema kwamba amefurahishwa na utaratibu mzima wa kupata kiwanja chenye hati, huduma zinazotolewa na Bayport, ambapo mteja hana jukumu lolote la kufuatilia hati katika maeneo yanayohusika.

“Utaratibu wa kununua kiwanja kasha ukapewa hati bila kufuatilia wizarani ni mpya, hivyo binafsi nimeufurahia na unaweza kuifanya Bayport kuwa moja ya ofisi zenye kujali muda na gharama za kiutendaji wa wateja wao,” alisema.

Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo ya bidhaa ikiwamo viwanja pamoja na fedha taslimu isiyokuwa na amana wala dhamana, huku taasisi hiyo ikiwa na matawi zaidi ya 82 nchi nzima kwa ajili ya kuwapatia Watanzania huduma bora.


 

Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akizungumza jambo baada ya kumkabidhi hati mteja wao Mary Simon kushoto baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Mikopo wa Bayport Financial Services, Nasibu Kamanda.
 

Mteja wa Bayport Financial Services Sixtus Kilenga kushoto akisaini kama sehemu ya kukabidhiwa hati ya kiwanja. Hati hizo kwa wateja walionunua viwanja vinavyopatikana kwa njia ya mkopo na fedha taslimu zinaendelea kutolewa kwa waliokamilisha taratibu zao.

No comments:

Post a Comment