Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, (aliyevaa miwani) akiwasikiliza
wakuu wa wilaya wastaafu ambapo Shigongo
aliowapa somo la ujasiriamali, aliyepeana nae mkono wa kwanza kulia ni Mkuu wa
wilaya mstaafu Bagamoyo, Brother. Ahmedi
Kipozi.
...............................................................................................................................
Wakuu wa wilaya wastaafu waanzisha SACCOS ili kukabiliana na changamoto
mbalimbali za kiuchumi.
Akitangaza azimio hilo, mwishoni mwa mafuno hayo yaliyofadhiliwa na Mfuko
wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es
Salaam, Mjumbe wa Sekretariati ya wakuu hao wastaafu, Crispin Meela, alisema,
wajumbe 10 wamechaguliwa na wana semina hao ili kushughulikia utaratibu mzima
wa kuanzishwa kwa SACCOS hiyo haraka iwezekanavyo.
Wajumbe wa Kamati ya muda ya kusimamia mambo hayo ni pamoja na Ramadhan
Maneno (Mwenyekiti), Betty Mkwasa (Katibu), Crispin Meela, Erasto Sima, Geogina
Bundala, Farida Mgomi, Said Amanzi, Fatma Ally, Muhingo Rweyemamu na Manzie
Mangochie.
Kwenye mafunzo hayo Wakuu hao wa wilaya wastaafu, waliweza kupata elimu
kutoka kwa wataalamu mbalimbali wakiwemo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’ Issa, na wataalamu wa Saikolojia, na Wajasiriamali
wenyewe kama vile Eric Shigongo.
Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, ametoa
changamoto kwa wakuu hao wanaokadiriwa kufikia 100 na ambao wamejiunga
uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kuwa uamuzi
wao utawakwamua kiuchumi na wanachotakiwa ni kuwa na mpango kamambe utakaoweza
kutekelezeka kwa ufanisi mkubwa.
kama shirika lingine lolote lile la kutoa huduma za Pensehni na za
kifedha, umoja huo ni fursa kubwa kwa Mfuko na ndio maana umeamua kuwaunga
mkono ili mmfikie azma yenu ya kuanzisha SACCOS hiyo”. Alisema.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akiwasilisha mada ya ujasiliamali, kwa wakuu wa wilaya wastaafu katika semina ya mafunzo ya ujasiliamali iliyofadhiliwa na mfuko wa pensheni wa PSPF na kufanyika makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es Salam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), George Simbachawene, (watatu waliokaa),
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, (wapili waliokaa),
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, George Yambesi, (wapili kulia),
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (wakwanza kushoto waliokaa) na
Mwenyekiti wa Wakuu hao wa Wilaya wastaafu, Ramadhan Maneno, (wakwanza kulia
waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wastaafu hao
Mkuu
wa Wilaya mstaafu, Christopher Kangoye
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akifunga mafunzo hayo Agosti 16, 2016
Meneja
wa PSPF, anayeshughulikia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Mwanjaa Sembe,
akitoa mada kuhusu faida za kujiunga na mpango huo.
Kaimu
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti
Lello, akitoa mada kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo hususan ushirikiano wa
Mfuko huo na PSPF, katoa bima ya afya kwa wanachama wa PSPF
Mkuu
wa Wilaya Mstaafu, Betty Mkwasa, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa
zikitolewa kwenye mafunzo hayo.
Mkuu
wa Wilaya Mstaafu, Manzie Manguchie, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa
zikitolewa kwenye mafunzo hayo.
Mwenyekiti
wa Wakuu wa Wilaya Wastaafu, Ramadhan Maneno, (kushoto), akizungumza jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publisher, Eric Shigongo
Mkuu
wa Wilaya Mstaafu, Makunga, akitoa maoni yake kuhusu uanzishwaji wa SACCOS hiyo
Meneja
wa PSS, Mwanjaa Sembe, akimsikiliza Mkuu wa wilaya mstaafu, Erasto Sima.
Shigongo
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wastaafu, baada ya
kuwapa elimu juu ya ujasiriamali.
Kaimu
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Mkoa wa Ilala, Hipoliti
Lello, (kushoto), akizungumza jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul
Njaidi, (kulia) na Mtafiti wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mapesi Maagi
No comments:
Post a Comment