Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,
Maj. Gen. Gaudence Milanzi ametoa wito kwa wadau wauhifadhi nchini kukemea kwa
nguvu zote tabia ya uingizaji wa mifugo ndani ya hifadhi za Misitu na
Wanyamapori nchini kwakuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi na kunahatarisha
ustawi wa hifadhi hizo ambazo ni muhimu kiikolojia na uchumi na wa taifa.
Milanzi ametoa wito huo juzi wakati akifunga
mafunzo maalum ya kijeshi katika kituo cha Mlele ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Katavi, Mkoani Katavi kwa Mameneja wa Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro na Askari wa TANAPA kwa ajili kubadilisha mfumo wa utendaji katika taasisi hizo kutoka wa kiraia kwenda wa Jeshi Usu (paramilitary) kuboresha utendaji wao wa kazi.
ya Ngorongoro na Askari wa TANAPA kwa ajili kubadilisha mfumo wa utendaji katika taasisi hizo kutoka wa kiraia kwenda wa Jeshi Usu (paramilitary) kuboresha utendaji wao wa kazi.
“Mifugo katika hifadhi zetu sio sahihi ni kinyume
kabisa chasheria za nchi, endeleeni kulikemea hili, tusipige siasa
kufurahishana kwakua madhara yake ni mengi ikiwemo uharibifu wa vyanzo vya
maji, muingiliano wa magonjwa baina ya mifugo na wanyamapori na kuharibu ubora
wa vivutio vyetu” Alisema Milanzi.
Sheria ya Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009
Ibara ya 18 (2) inakataza kabisa kuingiza mifugo ndani ya hifadhi, Sheria hiyo
inasema “Si ruhusa mtu yeyote kuingia na kulisha mifugo ndani ya Mapori
ya Akiba, Mapori Tengefu na Ardhioevu”.
Milanzi alisema kuwa hifadhi za taifa nchini
zina umuhifu mkubwa kwa uchumi wa taifa kwakuwa kupitia utalii zinachangia
asilimia 17.5 ya pato la taifa na asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za nje
(foreign currency). Aidha sekta hiyo inatoa ajira zaidi ya milioni moja na nusu
kupitia huduma za kitalii nchini.
Mbali na faida za kiuchumi hifadhi hizo pia
zina faida nyingi za kiikolojia ambazo ni uhifadhi wa vyanzo vya maji, kusaidia
upatikanaji wa mvua na hewa safi kwa viumbe hai ikiwemo binaadamu. Alisema
kuharibu hifadhi hizo kwa kulisha mifugo ndani yake ni jambo ambalo halikubaliki
kwa kuwa ni kuhatarisha pia maisha ya binaadamu ambayo yanategemea hifadhi
hizo.
Alieleza kuwa Serikali inaenda kulifanyia kazi
tatizo hilo pamoja na migogoro mingine ya ardhi kwa ajili ya kuyatafutia suluhu
kwa kushirikisha Wizara zinazohusika ambazo ni Ardhi, Kilimo na Mifugo, Sheria
na Katiba, Tamisemi, Maliasili na Utalii na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo,
Milanzi alisema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uadilifu, nidhamu, ujasiri,
uaminifu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa muda mfupi na hivyo kuwataka
kuyatumia kuongeza ufanisi katika kulinda maliasili zilizopo kwenye maeneo yao.
Aliwataka pia wahitimu hao kutafsiri mafunzo
hayo na maendeleo ya sekta ya uhifadhi nchini na kuliongezea taifa mapato kwa
kuboresha huduma za utalii, kubuni bidhaa mpya za utalii na kuboresha mfumo wa
ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi aliwataka wahitimu hao kutumia
mafunzo waliyoyapata kuziba mianya yote ya ujangili na kwamba jamii inategemea
kuona kazi hiyo kwa vitendo.
Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na UNDP kupitia
mradi wa “Spanest” yalifanyika kuanzia tarehe 15 Julai hadi tarehe 13 Agosti,
2016 kwa kuwahusisha washiriki 69 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na
Tanapa. Mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa awamu yanatemewa
kuhusisha taasisi zote za uhifadhi wa wanyamapori nchini kuelekea kwenye mabadiliko ya muundo wa utendaji kazi kutoka mfumo wa Kiraia kwenda mfumo wa Jeshi Usu (Paramilitary).
kuhusisha taasisi zote za uhifadhi wa wanyamapori nchini kuelekea kwenye mabadiliko ya muundo wa utendaji kazi kutoka mfumo wa Kiraia kwenda mfumo wa Jeshi Usu (Paramilitary).
No comments:
Post a Comment