Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel akielezea jambo mara baada ya kutia saini katika kitabu cha wageni
ofisini kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC)
Padre Raymond Sabas (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji
Habari Kanisani jana Jijini Dar es Salaam. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini
Media Padre Joseph Matumaini.
.............................................................................
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole
Gabriel amewataka wanahabari nchini kuandika na kuripoti habari kwa jamii
ambazo zina ukweli na zinazotoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo.
Prof. elisante Ole Gabriel ameyasema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho
ya siku ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika jana Kurasini Jijini
Dar es Salam ambapo amesema wanahabari nchini wanapaswa kutumia vyema taaluma
yao na maadili ya uandishi wa habari.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema kuwa ni vyema wanahabari kwenda na
mabadiliko ya teknolojia kwa kuitumia vizuri katika masuala ya kutoa
habari kwa jamii bila kuathiri Utamaduni na amani iliyopo nchini.
“Kuweni makini katika matumizi ya teknolojia katika kile mnachotaka
kuandika ili mlinde Utamaduni wetu,yale yanayokwenda kwa jamii muyachuje na
lazima muyajue vizuri na kwa usahihi ili kuepuka matokeo hasi kwa
jamii”.Alisema Prof.Elisante Ole Gabriel.
Kwa upande wake Padri Joseph Matuamaini ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Tumaini Media amesema kuwa vyombo vya habari lazima viwe na Sera na Dira
ambayo inaeleweka kwa watazamaji ili iwe rahisi kuelewa ujumbe wanaoufikisha.
“Vyombo vya habari vya kidini kuweni na huruma kama Baba wa Mbinguni
,lazima mufikishe ujumbe kwa jamii kuhusu Utukufu wa Mungu na umuhimu wa amani
ili kuondoa hofu kwa wananchi”.Alisema Padri Matumaini.
Padri Mtumaini ameongeza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya
kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa Serikali kuhamia Dodoma ili kuondoa hofu
iliyoingia moyoni mwao kuwa itadhorotesha maendeleo.
Rais alipotangaza Serikali kuhamia Dodoma wananchi waliingiwa na
hofu,lakini hakuna sababu ya kuogopa bali tuamini kuwa ni hatua nzuri ya kuleta
maendeleo na kutimia kwa ndoto ya muda mrefu ya Taifa letu.
Maadhimisho hayo yalibeba pia ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa Francis
mabao umesisitiza namna bora ya kutumia mawasiliano katika kutangaza
mambo mazuri ya Mungu kwa jamii.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel akisisitiza jambo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 50 ya
Upashanaji Habari iliyofanyika katika ukumbu wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa
Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa
TEC Padre Raymond Saba, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya TEC Bw.
Bernard James na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowassa wakati
wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi
wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki jana Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini akifafanua jambo alipokuwa
akiwasilisha ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa Fransisko kuhusu maadhimisho ya 5O
ya siku ya Mawasiliano duniani jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya washiriki katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani
yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC)
wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika maadhimisho hayo jana Jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment