Kamishna wa TRA
Bw. Alphayo Kidata akipata maelezo kutoka kwa Rehema Shayo Meneja wa Usajili
TRA wakati akikagua utekelezaji wa uhakiki huo.
...........................................................................................................
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imezindua zoezi maalumu kwa ajili ya
kuhakiki na kuboresha taarifa za usajili wa namba za utambulisho wa mlipa kodi
(TIN).
Uzinduzi huo umefanywa na Kamishna Mkuu wa Ofisi hiyo Bw, Alphayo
Kidata kwa kushirikiana na wafanyakazi wa ofisi hiyo mapema hii leo jijini Dar
es salaam, ambapo kuanzia sasa zoezi hilo litakuwa endelevu katika mikoa yote
ya Tanzania bara na visiwani .
Kidata alisema kuwa lengo kubwa la uzinduzi wa zoezi hilo ni kubadili mfumo wa sasa wa kuhifadhi kumbukumbu za walipa kodi kwa kuweka mfumo mpya unaoendana na ukuaji wa teknolojia ambao utakuwa na walipa kodi wake wanaostahili kuwepo kwenye wigo.
Aidha aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia kuwaondoa walipa kodi hewa ,kuongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi wa ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu na kuwezesha ulipaji kodi kuwa nafuu kwa mlipaji.
Hata hivyo katika hatua nyingine Kidata ametoa wito kwa yeyote mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi kufika katika ofisi za mamlaka hiyo ili kuweza kupata utaratibu wa zoezi zima jinsi linavyokwenda.

No comments:
Post a Comment