Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo amepiga marufuku matumizi ya mafuta ya transfoma kwa ajili ya kukaangia
chips na kutengeneza mikorogo.
Profesa Muhongo ameyasema hayo alipokuwa
akihutubia wakazi wa kijiji cha Kirongo wilayani Muheza mkoani Tanga katika
ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) katika mkoa huo.
Prof. Muhongo
alisema mafuta hayo hayakutengenezwa kwaajili ya kula hivyo kuyatumia
kwaajili ya chakula ni kuhatarisha afya za
walaji na kwamba yeyote atakabainika
kutumia mafuta ya Transfoma hatua zakisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Aidha, amepiga
marufuku pia utumiaji wa mafuta hayo ya
Transfoma kuchanganyia na v
ipodozi kaarufu kama Mkorogo, na kusema
kuwa matumizi ya aina hiyo yanatarisha
afya za watu.
Kumekuwa na
uvumi wa muda mrefu kuwa, baadhi ya wakaanga chipsi
wamekuwa wakitumia mafuta ya Transfoma
kuchanganya na mafuta ya kula kawaida
kwa madai kuwa kwakufanya hivyo hutumia
mafuta ya kula kidogo na kuongeza faida
katika biashara zao.
Wakati wakaanga Chipsi wakitumia mafuta
hayo ya Transfoma kukaangia chipsi, watumiaji
wa vipodozi nao wamekuwa wakitumia mkorogo (mchanganyiko maalum) unaochanganywa
na mafuta ya Transfoma.
Hali hiyo huwenda ndiyo inayopelekea mara kadhaa Mafuta ya Transfoma huripotiwa kuibiwa na kuacha baadhi
ya maeneo kukaa bila ya umeme huku
serikali ikipata hasara ya kujaza mafuta mengine kwenye Transfoma.
No comments:
Post a Comment