TAREHE 21.08.2016 MAJIRA YA 10:00 USIKU KATIKA ENEO LA CLUB YA VILLA PARK
RESORT KATA YA KIRUMBA WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, ASKARI NAMBA G.5092 PC
JOHN NYANGE WA OFISI YA MKUU WA UPELELEZI NA MAKOSA YA JINAI MKOA WA MWANZA
(RCO), ALIUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI ENEO LA SHINGONI NA MTU
ALIYEKUWA ANAUGOMVI NAE.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUA NA UGOMVI WA MUDA MREFU NA MTU
ALIYEJULIKANA KWA JINA MAGINA HUSSEIN MIAKA [27] FUNDI COMPUTER MSUKUMA NA
MKAZI WA MTAA WA KIGOTO, AMBAPO MAREHEMU ALIKUWA AKIMDAI BWANA MAGINA HUSSEIN
COMPUTER AINA YA LAPTOP.
NDIPO USIKU WA LEO MAJIRA TAJWA HAPO JUU
WALIKUTANA ENEO LA CLUB YA VILLA PARK HUKU MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO IKISEMEKANA
KUWA ALIKUWA NA WENZAKE WATANO NDIPO WALIMVAMIA NA KUMCHOMA NA KITU CHENYE NCHA
KALI SHINGONI NA KUFARIKI DUNIA NJIANI WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALI.
MAREHEMU KWA SASA ALIKUWA NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA STEFANO MOSHI
MEMORIAL UNIVERSITY COLLEGE CHA MJINI MOSHI, ALIKUWA ANASOMEA SHAHADA YA
SAYANSI YA HABARI NA MAWASILIANO MWAKA WA PILI, AIDHA ALIREJEA MWANZA BAADA YA
KUPATA LIKIZO KUJA KUIANGALIA FAMILIA YAKE NDIPO UMAUTI UKAMKUTA.
WATUHUMIWA SITA AKIWEPO MAGINA SELEMANI AMBAYE ALIKUWA NA UGOMVI NA
MAREHEMU PAMOJA NA WENZAKE WATANO WAMEKAMATWA, WAPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI
LA POLISI HUKU UCHUNGUZI KUHUSIANA NA KIFO HICHO UKIWA BADO UNAENDELEA,
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATAFIKISHWA MAHAKAMANI,
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA
UCHUNGUZI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI
ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWAMBA JESHI LA POLISI MKOA
WA MWANZA LIMESIKITISHWA NA KIFO CHA ASKARI HUYU KWANI LIMEMPOTEZA ASKARI
KIJANA AMBAYE BADO JESHI LILIKUWA LINAMTEGEMEA.
LAKINI PIA ANAWATAKA WATU WENYE
TABIA ZA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUWAPIGA WENGINE HADI KUFIKIA KUPOTEZA
MAISHA KUWA WANAFANYA KOSA LA JINAI, NA KAMA WATU WANADAIANA WAFUATE TARATIBU
ZA KISHERIA ZILIZOWEKWA ILI KUEPUSHA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA, HIVYO JESHI LA
POLISI LINAWATAKA KUACHA TABIA HIYO MARA MOJA KWANI HATUA KALI ZA KISHERIA
ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WAPOLISI (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment