Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd anayejenga jengo
la pili la abiria wakati alipokagua uwanja wa kimataifa wa Songwe, Mkoani
Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifanya ukaguzi wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe , Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) kuhusu
ujenzi wa jengo la pili la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, wakati
alipokagua uwanja huo Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa
michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege (TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata
maelezo kutoka kwa Bw. Baraka Mwambipile kuhusu namna ndege zinavyoongozwa
wakati wa kuruka na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe, Wakati
alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata
maelezo ya mfumo wa utabiri wa hali ya hewa katika Uwanja wa Kimataifa wa
Songwe (SIA) kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya hali ya hewa uwanjani hapo,
Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
....................................................................................................................................
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema
kuwa Serikali haitaendelea na ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja
wa ndege wa Songwe uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa
kuchunguza ili kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi
huo.
Prof. Mbarawa alitoa kauli hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo
linalojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema
hadhi ya jengo hilo hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu
zote zilifuatwa kabla ya ujenzi.
Alibainisha kuwa, kazi ya tume hiyo ya wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa
kumpata mkandarasi ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa
kwa mkandarasi kama inaendana na thamani ya jengo hilo.
“Serikali haiwezi kutoa fedha ya kumalizia jengo hili kabla ya
kujiridhisha ili kuhakikisha fedha tutakazozitoa zitatumika kulingana na
ilivyopangwa na thamani ya fedha inaendana na jengo lenyewe”, alisema Waziri
Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa alieleza ili kuwa na miundombinu imara
na ya kudumu ni lazima kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa
vizuri na taratibu za kupata mkandarasi bora zinafuatwa.
“Kutokuwa na miundombinu isiyo imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele
maslahi binafsi na siyo ya Taifa”, alisisitiza Waziri, Prof. Mbarawa
ambapo aliutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
kuhakikisha makosa yaliyojitokezo kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika
uwanja wa ndege wa Mwanza hayajirudii katika kiwanja hiki.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri
amemhakikishia Waziri Mbarawa kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu
na makubaliano yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.
Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa,
Njombe na Ruvuma na katika mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi
bilioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani
hapo.
No comments:
Post a Comment