Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid hemed Mwanga.
................................................................................................................................
Watumishi wa serikali wilayani Bagamoyo
wanaokwepa kufanya usafi wa mazingira
kwa pamoja, wametakiwa kuacha tabia hiyo vinginevyo watafute wilaya nyingine.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga
alipokuwa akizungumza na wananchimara baada ya kumaliza kufanya usafi leo
katika mji wa Bagamoyo.
Majid alisema kuwa swala la kufanya usafi wa
mazingira ni swala la kitaifa kutokana na agizo la mheshimiwa Rais Magufuli
hivyo kukwepa zoezi hilo ni kukwepa agizo la Rais na kuongeza kuwa, yeye hatavumilia kumuona mtumishi anakaidi amri halali ya
serikali.
Aidha, ameonya piya tabia ya watumishi wa
serikali kukaidi maagizo mbalimbali yanayotolewa na wenyeviti wa vitongoji na kusema
kuwa hao ndio viongozi wa serikali ngazi ya mitaa wanapaswa kuheshimiwa.
Majid ameyasema hayo kufuatia taarifa ya aliyopewa kuwa baadhi ya
watumishi wa serikali katika mitaa
wanayokaa hawataki kuchangia gharama za
kusafirisha taka utaratibu ambao
umewekwa na serikali za vitongoji katika
kukabiliana na tatizo la uchafu, kwa kuzingatia kuwa Halmashauri ya
Bagamoyo haina gari za kutosha kusafirisha taka.
Amemuagiza Afisa utumishi wa Halmashauri ya
Bagamoyo kuchunguza watumishi ambao hawataki kutii mamlaka za wenyeviti kwa
kuchangia gharama za kusafirisha taka awatoe kwenye nyumba za serikali ili
wawekwe watumishi wenye kutii mamlaka.
Aliongeza
kuwa wenyeviti wa vitongoji, watendaji kata na maafisa tarafa ni
viongozi halali katika maeneo yao hivyo
maagizo wanayotoa yanapaswa kuheshimiwa bila ya kujali wewe mkazi wa mtaa huo una
cheo gani.
"Hata mimi ninapokaa namuheshimu mwenyekiti wangu
wa kitongoji, namuheshimu Mtendaji kata
wangu na Afisa tarafa kwakuwa wao niviongozi halali hivyo nitapokea jambo
linalohusueneo langu ninaloishi ili nami nishiriki kama mkazi wa eneo hilo,
vipi wewe una mdharau mwenyekiti hata anapokutaka ushiriki kwenye usafi wa
mazingira" Alisema mkuu huyo wa wilaya.
Amewataka wenyeviti wa vitongoji kuwakamata
watumishi wanaopinga maagizo ya kufanya usafi
ili kuweka nidhamu ya
kutii viongozi wa serikali.
Aidha, amewaonya wananchi wenye tabiaya kukusanya taka na kuziweka bele nyumba bila
ya kuzisafirisha ambapo amewataka kufuata utaratibu uliowekwa na wenyeviti wa
vitongoji katika kusafirisha taka ili mji ubaki ukiwa safi.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa wilaya Bagamoyo
amesema kuwa kuanzia sasa usafiwa pamoja
mbagamoyo utafanyika kwa mwezi mara
mbili ili kuuweka mji safi.
Usafi huo wa mazingira mjini Bagamoyo ambao umeongozwa
na mkuu wa wilaya, umefanyika kwa
kushirikiana watumishi wa serikali, wananchi, wakawaida, wafanyabiashara, taasisi mbalimbali za serikali wakiwemo jeshi la
magereza, jeshi la Polisi, Mamlaka ya
Maji safi na maji taka DaresSalaam (DAWASA), Shirika la maji safi na maji taka
Dar es Salaam, (DAWASCO) Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF) na wadau
mbalimbali wa usafi wilayani Bagamoyo.
Wafanyakazi wa DAWASA wakimsikiliza mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga.
Askari wa jeshi la magereza wakimsikiliza mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo alipokuwa akiwahutubia
wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Majengo mara baada ya kufanya
usafi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment