Kitengo cha dharura cha kuitikia
matukio ya usalama kwenye mitandao nchini (Tanzania Computer Emergency
Response Team- TZ-CERT) kimepewa jukumu la kitaifa la kuratibu matukio ya
usalama katika mitandao kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kikanda na
kimataifa katika kusimamia matukio ya usalama mitandaoni.
TZ-CERT ilianzishwa kwa sheria ya Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta ya 2010, kifungu namba 124. Kifungu namba 5(1) cha
kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta zilizotolewa Desemba 2011,
kilielekeza uanzishwaji wa TZ-CERT ndani ya mfumo wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA). Huduma za TZ-CERT zilizinduliwa rasmi tarehe 17 mwezi May
mwaka 2015.
Majukumu makuu ya TZ-CERT kisheria ni kuwa kiungo
cha kitaifa nchini na kwa nchi za nje kwa masuala yote yanaohusiana na usalama
mtandaoni. Katika kutimiza wajibu wake TZ-CERT:
1.
Inatoa
ushauri wa kitaalamu wa kukabiliana na matukio ya kiusalama yanayotokea na
kuzuia madhara zaidi.
2.
Inafanya
uchambuzi wa taarifa za matukio ya usalama wa mtandao kutoka vyanzo mbalimbali,
kimataifa na kitaifa.
3.
Kutoa
mwongozo wa kitaalamu “Security Advisory” kwa umma na wadau katika
maeneo ambayo yameonekana kuwa na madhaifu.
4.
Uhamasishaji,
kuelimisha na kujenga uwezo (Awareness & Capacity Building) wa masuala
ya usalama wa mitandao kwa serikali na wadau kutoka sekta mbalimbali.
5.
Tathimini ya
udhaifu wa mifumo ya kompyuta (Vulnerability assessment) katika mitandao
ya wadau wa TZ-CERT.
Ikumbukwe kwa sasa Tanzania kuna watumiaji wa
mtandao wanaokadiriwa kufikia milioni Kumi na Saba (17 milioni) kutokea milioni
Tano (5 milioni) katika mwaka 2011.
Kutokana na uzoefu uliopatikana kwa muda wa mwaka
mmoja toka ianze rasmi kutoa huduma, TCRA imebaini pamoja na mambo mengine
ukosefu wa taarifa muhimu za usalama wa mitandaoni kumechangia kuwepo kwa
matukio ambayo yangeweza kuepukika.
2.
Kwa nini
kampeni ya kuongeza ufahamu?
Kampeni hii ya kuongeza ufahamu imekuja wakati
muafaka baada ya timu ya TZ-CERT kubaini changamoto nyingi na aina mbalimbali
za matatizo ya kwenye mtandao ambayo wanakutana nayo watanzania wengi kutokana
na ufahamu mdogo wa jinsi ya kujilinda mitandaoni, kulinda taarifa zao
mtandaoni pamoja na matumizi sahihi ya mtandao kwa ujumla wake.
3.
Kampeni
itawalenga watu gani?
Kampeni hii inawalenga watumiaji wa huduma za
Intaneti wa rika zote kuanzia watoto mpaka watu wazima.
4.
Kampeni
itahusisha nini?
Kampeni hii inazinduliwa rasmi leo tarehe 17 mwezi 8
mwaka 2016 na itaendelea kwa miezi mitatu. Hata hivyo kampeni za kuelekea
uzinduzi wa leo zilianza tarehe 01 Agosti, 2016. Kwa kuwa kampeni hii ni ya
matumizi ya mitandao itaendeshwa zaidi kwenye mitandao ambapo watumiaji wa
mitandao mbali mbali Tanzania watatumia muda wao kujifunza njia bora na salama
za matumizi ya mtandao.
Katika kipindi hiki cha kampeni wananchi watajifunza
mada mbali mbali ikiwa ni pamoja na matunzo sahihi ya kompyuta na programu
zake, taratibu za kutumia mitandao kwa usalama, matumizi sahihi ya namba au
neno la siri, sheria ya makosa ya mitandao, uwekaji wa taarifa kwenye mitandao
ya kijamii na matumizi sahihi ya mitandao kwa watoto.
Kampeni hii itatolewa katika akaunti za TZ-CERT za
mtandao wa facebook (https://www.facebook.com/Tz-Cert), twitter (https://twitter.com/tz_cert)
na instagram (https://www.instagram.com/),
pamoja na vyombo vya redio na TV kufikisha jumbe mbalimbali za kuelimisha
watumiaji wa mitandao na umma matumizi sahihi ya mitandao.
5.
MAMBO MUHIMU
YA KUZINGATIA UTUMIAPO HUDUMA ZA INTANETI/MITANDAO
1.
Kuwa makini
na taarifa za binafsi unazoziweka kwenye mitandao wa jamii.
1.
Ukisaidiwa
kuanzisha akaunti za mtandao wa kijamii, hakikisha unabadilisha neno la siri
lilotumika mara moja na neno hilo la siri usimshirikishe mtu yeyote.
- Usijibu jumbe unazopokea kwenye akaunti yako ya barua pepe unaokutaka kuhakiki taarifa zako.
1.
Usijibu
ujumbe wowote wa barua pepe unaokueleza kuwa umeshinda bahati nasibu.
1.
Usifungue
kiambatisho au kubofya kiungo (link) unayotumiwa na mtu usie mjua kabla ya
kuhakikisha uhalali wa barua pepe husika.
Ili kujiepusha na kukiuka sheria mbalimbali za
mawasiliano ya mtandao umma wote unashauriwa kuzingatia yafuatayo:
1.
Usitunge na
kusambaza ujumbe wa maudhi, uzushi au uchochezi.
1.
Usiendelee
kusambaza ujumbe wa chuki, maudhi au uchochezi unaopokea kutoka kwa mtu
mwingine. Badala yake ufute mara uupokeapo au toa taarifa.
- Usitembelee tovuti na blogu za ponografia/ngono,
1.
Usitengeneze
akaunti za mitandao ama kwa lengo la kufanya utapeli, ulaghai au kwa kutumia
taarifa zisizo zako.
1.
Tunza vifaa
unavyohifadhia kumbukumbu zako.
- Uzinduzi wa tovuti mpya ya TZ-CERT
Pamoja na uzinduzi wa kampeni hii, pia tovuti mpya
ya TZ-CERT itazinduliwa rasmi leo. Tovuti hii yenye lugha ya kingereza na
Kiswahili itaanza kutumika rasmi kutoa taarifa muhimu za kuwasaidia wananchi
kujilinda na matukio ya kwenye mitandao. Tovuti hii pia hutumika kutuma na
kutoa taarifa ya matukio mbali mbali kwa TZ-CERT kwa msaada wa kitaalamu.
Anwani ya tovuti hizi ni www.tzcert.go.tz
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mawasiliano Towers
20 Bara Bara ya Sam Nujoma
S.L.P. 474
14414 DAR ES SALAAM
17 Agosti 2016
No comments:
Post a Comment