Wa kwanza kushoto ni Diwani wa viti maalum Tarafa ya Miono, Mh. Sijali Mpwimbwi, wa pili kushoto ni Diwani wa viti maalum Tarafa ya Chalinze, Mh. Mwanakesi Madega, wa tatu ni Diwani wa kata ya Kimange, Mh. Hussein Hading'oka, anaefuata ni Diwani viti maalum Tarafa ya Kwa Luhombo Mh. Tunu Mpwimbwi, kutoka kulia wa kwanza ni Diwani wa kata ya Msata, Mh. Cham Semiono wa pili kulia ni Diwani wa kata ya Lugoba, Mh. Rehema Mwene na wa tatu kulia ni Diwani wa kata ya Kibindum,Mh. Mkufya Ramadhani Mkufya.
.....................................................................................
Halmashauri mpya ya Chalinze imejipanga kusimamia
Bajeti ya Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha
zilizotengwa kwaajili ya wanawake na vijana zinafika kwa walengwa
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Chalinze Mh. Saidi Zikatimu wakati
wa kikao cha kufunga taarifa ya robo ya nne ya mwaka 2015/16. katika
ukumbi wa Halmashauri ya Chalinze.
Halmashauri ya chalinze ambayo imeanzishwa kutoka
Halmashauri ya Bagamoyo, imemaliza bajeti iliyoandaliwa na Halmashauri ya
Bagamoyo ambapo sasa Chalinze itaanza bajeti inayojitegemea kama Halmashauri
mpya na hivyo kufanya wilaya ya Bagamoyo kuwa na Halmashauri mbili, Halmashauri
ya Bagamoyo na Halmashauri ya Chalinze ndni ya wilaya moja ya Bagamoyo.
Akielezea mikakati ya Halmashauri hiyo,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze
Mh. Saidi Zikatimu alisema Halmashauri ya Chalinze kupitia Madiwani wake
imejipanga kuhakikisha Bajeti
iliyopangwa inatekelezeka kwa kusimamia vizuri mapato na matumizi ya
Halmashauri hiyo.
Aidha, alisisitiza kuwa madiwani wa Halmashauri
hiyo mpya, wamejipanga kusimamia
utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri na
kuongeza kuwa kila fedha itapelekwa kwenye
matumizi yake yaliyopangwa na si vinginevyo.
Alisema, katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu
yao kwa maslahi ya wananchi, Baraza
hilo litahakikisha fedha zote
zilizotengwa kwaajili ya wanawake na watoto zinafika kwa walengwa.
Aidha, Mwenyekiti huyo huyo wa halmashauri
alimshukuru Mbunge wa Jim bo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete, kwakuwa fedha
za mfuko wa jimbo zimeshafika kwenye
vikundi na kuanza kuzifanyia kazi.
Katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani piya
wamejadili uhaba wa walimu uliopo katika shule za Halmashauri hiyo ikiwa
ni pamoja kuwapa uhamisho bila ya sababu
za msingi ambapo wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kutoa taarifa kwa
baraza la madiwanni kwa mabadiliko ya walimu ili kwa pamoja waweze kuangazia sehemu
yenye uhitaji wa walimu na kuepuka walimu kuchagua sehemu za mjini na kuacha
shule za vijijini zikiwa hazina walimu.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambae ni mjumbe wa
Baraza la madiwani, Mh. Ridhiwani Kikwete alimtaka Mkurugenzi kuacha kuwapangia walimu kwa upendeleo na badala
yake kwa pamoja washirikishane kuona sehemu zenye uhitaji wa walimu.
Kwa upande
wake Diwani wa Kata ya Kimange, Mh. Husein Hading'oka alisema umakini unahitajika
katika swala la kuhamisha na kuwapangia walimu vituo vya kazi ili kuepuka
kuweka walimu wengi katika shule moja na kuziacha baadhi ya shule zikiwa hazina walimu wa
kutosha.
Aidha, Baraza hilo limejadili swala la msamaha wa
ushuru kwa wawekezaji wanaotumia kokoto kwenye machimbo ya Chalinze ambapo
wamekataa misamaha hiyo kwakuwa
itavuruga Bajeti ya Halmashauri.
Wkichangia hoja katika kikao hicho Madiwani
hao walisema swala la msamaha wa ushuru
wa kokoto kwa wawekezaji wanaochukua kokoto katika machimbo ya Chalinze
linahitaji kuzingatia Mahitaji ya Bajeti
ya Halmashauri ambayo tayari imeshapitishwa.
Walisema, endapo baraza litapitisha msamaha kwa
baadhi ya wawekezaji walioomba kusamehewa itavuruga bajeti hiyo na kutaka baraza hilo lisipitishe msamaha huo kwa mwaka
huu na kama ikibidi liangaliwe kwa mwaka wa fedha ujao.
Kufuatia hoja hizo wajumbe wa baraza, Mwenyekiti
wa Halmashauri Mh. Saidi Zikataimu aliridhia na kusema kuwa, pamoja na
kuheshimu michango ya wawekezaji hao Halmashauri inaweza kutetereka mapato yake
ikiwa watapitisha misamaha hiyo na kuwataka wawekezaji hao kuendelea kulipa
ushuru kama kawaida kwa kuwa ni utekelezaji wa agizo la Bunge na serikalikwa
ujumla katika swala la kukusanya ushuru
ili Halmashauri ziweze kukusanya
mapato ya ndani kwa ufanisi.
Mwnyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mh. Saidi Zikatimu wa kwanza kulia, katikati ni Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Erika Liyegela na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.
Diwani wa kata ya Lugoba Mh. Rehema Mwene akitoa hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Miono, Mh. Juma Mpwimbwi akitohoja kwenye kikao cha kufunga Taarifa ya robo ya nne ya mwaka 2015/16. Waliokaa kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Ubena, Mh. Nicholous George Muyuwa, anaefuata ni Diwani wa kata ya Kiwangwa Malota Kwaga.
Aliyesimama ni Diwani viti maalum Msoga, Mh. Maria Moreto akitoa hoja kwenye kikao hicho, waliokaa kutoka kulia ni Diwani viti maalum Tarafa ya Msata, Mh. Rehema Mno, anaefuata ni Mh. Cham Semiono, Diwani wa kata ya Msata na watatu kutoka kulia ni Mh. Rehema Mwene Diwani wa kata ya Lugoba.
Aliyesimama ni Mh. Lekope Laini Langw'esilo, Diwani kata ya Pera, akichangia hoja katika kikao hicho.
Aliyesimama ni Diwani viti maalum Tarafa ya kwa Luhumbo, Mh. Tunu Mpwimbwi akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani Chalinze.
Mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wamikutano wa Halmashauriya Chalinze.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Erika Liyegela, wa katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mh. saidi Zikatimu na wa mwisho kulia ni M kurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa.
Kushoto ni Diwani wa kata ya Bwilingu, Mh. Lukas Lufunga na kulia ni Diwani wa kata ya Msoga, Mh. Hassan Rajabu Mwinyikondo.
No comments:
Post a Comment