Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akimkabidhi
moja ya dawati kati ya 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Karikoo wenye
asili ya China ,kwa Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema leo jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla fupi
ya kukabidhiwa madawati 200 kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili
ya China leo jijini Dar, kwaajili ya
shule ya msingi Maghorofani iliyopo Gongolamboto, jijini Dar Es Salaam. Wafanyabiashara
hao waliahidi kumkabidhi Mh. DC Mjema
Madawati 200 lakini leo wamekabidhi nusu ya madawati hayo (100), huku mengine
yakiendelea kutengenezwa. Shule hiyo ya Maghorofani ilikuwa na uhitaji wa
madawati 525, yakapatikana madawati 250
na kupungukiwa madawati 275.
Muwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania,Gou Haodong akizungumza
kwa ufupi mbele ya Waalimu,wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),kabla ya
kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariako wenye asili
ya China jijini Dar,pichani kulia ni Mkuu wa Wa Wilaya ya Ilala,Mh Sophia
Mjema.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule hiyo ya Maghorofani wakiwa wamekalia
baadhi ya madawati yaliyotolewa na Wafanyabiashara wa Kariakoo wenye asili ya
China jijini Dar.
No comments:
Post a Comment