SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kuwatangazia wateja wake
wote wa Wilaya
ya Bagamoyo kuwa, kutokana na kukatika kwa waya wa
mawasiliano, (Optic Fiber) kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, Ofisi ya Shirika
hilo wilayani Bagamoyo bado inashindwa kutoa huduma za kupokea malipo na kuuza
LUKU kwa muda mpaka hapo waya huo utakapoungwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Uhusiano MakaoMakuu yaTANESCO, Kwa sasa
Shirika linawaomba wateja wake wanaotaka kununua umeme au kulipia huduma
zingine za umeme kutumia njia mbadala ya mitandao ya Simu na makampuni mengine
yenye mikataba na TANESCO.
Jitihada zinaendelea ili kuhakikisha mkongo huo wa mawasiliano unaungwa
mapema
iwezekanavyo. Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu
wowote uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment