Mkurugenzi Mkuu kutoka kampeni ya Puma Energy Tanzania Ltd,Philippe
Corsaletti akimkabidhi tuzo/zawadi ya Begi na cheti mwanafuzi wa darasa la sita
kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent baada ya kuibuka mshindi wa
kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama
barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016, hafla
hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema
leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
Mashindano hayo
yalihusisha shule kumi kwa upande wa Dar Es Salaam ambazo ni Mwananyamala, Kisutu,Bunge,Kisiwani, Mchangani, Mnazini, Mwananyamala
B, Mikocheni, Mtendeni, Kisutu, Kisiwani na Ungindoni, Shule nyingine tatu ni kutoa
mkoa wa Geita ambazo zitashiriki na mchakato wa kuwapata washindi, matokeo ya
washindi wa mwisho yatatangazwa wakati wa kilele cha cha wiki ya Usalama
barabarani ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni
Zawadi ya heshima (tuzo) ambayo imetolewa na kampuni ya Puma Energy
Tanzania na kukabidhiwa kwa mshindi wa kwanza, Mwanafunzi wa darasa la sita
kutoka shule ya Msingi Bunge, Veronika Inocent.
Mwanafuzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge, Veronika
Inocent akilia kwa furaha mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele
cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika
shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016, hafla hiyo fupi
iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika
viunga vya shue ya msingi Bunge.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, (DCP) Mohamed Mpinga pamoja na
Waandaaji kutoka kampuni ya Puma Energy Tanzania na AMEND wakitafuta washindi
watatu wa shindano la uchoraji katika masuala mazima ya kuhamasisha usalama
barabarani 2016.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi
(DCP) Mohamed Mpinga akimkabidhi Mwanafunzi wa darasa la sita, Shaaban zawadi
ya Begi na Cheti,kutoka shule ya msingi Bunge baada ya kuibuka mshindi wa tatu
katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama
barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla
hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema
leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi,
(DCP) Mohamed Mpinga akimkabidhi Mwanafunzi wa darasa la sita Antonia Anthony
zawadi ya Begi na Cheti,kutoka shule ya msingi Mwananyamala baada ya kuibuka
mshindi wa pili katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha
usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka
2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania
ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
Picha ya Pamoja na Washindi watatu shindano la Uchoraji kwa ajili ya
kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa
mwaka 2016.
Baadhi ya Wanafunzi walioshiriki na kuibuka na zawadi kutoka Kampuni ya
Puma Energy Tanzania .
Mkurugenzi Mkuu kutoka kampeni ya Puma Energy Tanzania Ltd,Philippe
Corsaletti alisema kuwa shindano hilo linalenga kusaidia kuelimisha Wanafunzi
wa shule za msingi katika masuala ya Usalama barabarani. "Mpangp wetu
wa usalama barabarani kwa mashule hapa Tanzania ulianza toka mwaka 2013 na
mpaka sasa shule za msingi zipatazo 30 zimeshiriki,ikiwa ni jumla ya wanafunzi
38,638", alisema Philippe.Alisema kuwa shindano hilo pia linalenga
kumpatia Mwanafunzi nafasi ya kushiriki mawazo.
No comments:
Post a Comment