Mkuu wa mkoa wa Pwani injinia, Everist Ndikilko.
....................................................................................
Vijana wametakiwa kuacha tabia ya kukaa vijiweni na badala yake wajitume
katika kuifanya kazi ilikujipatiamaendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikiro wakati
wa sherehe za ufunguzi rasmi wa programu ya kambi ya vijana ya
kuwafundisha masuala ya kilimo na maarifa ambayo ipo chini ya
mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto rufiji (RUBADA) iliyofanyika
katika kijiji cha Mkongo.
Ndikilo amebainisha kwamb serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.
John Pombe Magufuli isingependa kuona vijana wa kitanzania hawataki
kutumia fursa zilizopo na kuamua kujiingiza katika vitendo ambavyo vipo kinyume
na taratibu na sheria za nchi.
Naye mwakilishi wa shirika la chakula duniani (FAO) nchini Tanzania
Fred Kafeero amesema kwamba kulingana na ripoti zinaonyesha asilimia 70
ya vijana katika africa hawana ajira hivyo kunahitajika juhudi za
makusudi za kuweza kuwasaidia katika kilimo cha mboga mboga,huku Mkuu wa Wilaya
ya Rufiji Juma Chwayo akiwaomba vijana hao kutumia fursa ya kilimo kupitia
mafunzo watakayoyapata.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa ameutaka
uongozi wa RUDABA kuhakikisha kwamba wanaepukana na malalamiko ambayo yalikuwa
yanatolewa dhidi yao na badala yake waweke mikakati endelevu ya kuwasaidia
vijana kujiendeleza zaidi pamoja na kuongeza juhudi za ujenzi wa
viwanda kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza uchumi.
Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao watanufaika na profamu hiyo akiwemo
Saimoni Nyimmba pamoja na Joseph Bada wamesema kwamba mafunzo hayo ya
kilimo na maarifa pindi watakapomaliza yataweza kuwasaidia
kuwapatia kipato pamoja na kuachana na suala la kuwa tegemezi
sambamba na kuondokana na kile kilimo cha kizamani.
MAFUNZO hayo ya kilimo na maarifa yataweza kuwanufaisha vijana wapatao
200 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambapo kwa sasa yataanza kuwanufaisha
vijana 62 kutoka katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo ujuzi watakaupata
wataweza kupata fursa ya kujiajiri wao wenyewe na kuleta mabadiliko chanya ya
kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment