Waziri
wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye akizungumza wakati
wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini
Dar es Salaam ulikuwa ukijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara
la Afrika na China.
................................................................
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye
amewataka waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa kuandika habari za
maendeleo ya bara la Afrika.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum na kueleza kuwa uhusiano baina
ya Afrika na China ni wa muda mrefu na umejikita katika kuboresha teknolojia ya
mawasiliano na hivyo kukuza uchumi wake.
Aidha aliongeza kuwa ili bara la Afrika liweze kuelezea historia
yake kwa mataifa mingine katika kujiletea maendeleo kuna haja
ya kuvijengea uwezo vyombo vya habari katika kutoa habari nzuri zenye manufaa kwa
jamii husika.
“Katika karne hii tuliyopo sasa kuna mabadiliko mengi ya
teknolojia hivyo ni budi kuendelea kuimarisha ushirikiano
ulipo baina ya China na Afrika ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii zetu
kupitia vyombo vya habari huku tukitunza na kueneza tamaduni zetu”
alisema Mhe.Nape.
Waziri Nape alizidi kufafanua kuwa vyombo vya habari katika nchi za bara
la Afrika vina uwezo mkubwa wa kukuza na kueneza utamaduni,
kuhudumia jamii,kujenga umoja wa kitaifa na kulinda maslahi ya
jamii duniani.
Naye Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing amesema
kuwa anafurahishwa na uhusiano uonaozidi kuimarika baina ya nchi za
Afrika na China na kuahidi kuboresha mawasiliano na mahusiano ili kufikia
mafanikio makubwa yaliyokusudiwa.
Mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum umejikita katika
kujadili mambo mbalimbali ikiwemo mahusiano baina ya mtu na mtu na Vyombo vya
habari,afya,na tiba asilia.
Rais
wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing akiwasilisha hotuba yake
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo
jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadali masuala mbalimbali ya ushirikiano baina
ya Bara la Afrika na China.
Mshauri
wa mambo ya Mawasiliano kutoka Tume ya Umoja wa Afrika Bibi. Doreen Apollos
akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public
Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili
uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na
afya.
Waziri
wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (kushoto)
akijadiliana jambo na Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li
Zhaoxing(kulia) wakati wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum
leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa
Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (wa kwanza kulia) na Balozi wa China
nchini Bw. Lv Youqing(wa pili kulia) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na
mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape
Mosses Nnauye(hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) na Balozi wa China nchini
Bw. Lv Youqing(kulia) wakionyesha hundi ya shilingi milioni arobaini na
tano zilizotolewa na watu wa China kwa ajili ya kuchangia madawati katika
shule za msingi za Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment