Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (katikati alie simama) akiwa katika
picha ya pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Msham Munde,
mkuu wa wilaya hiyo Filberto Sanga, na mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke mara
baada ya kukabidhi madawati 537 ya mbunge wilayani humo.
Sehemu ya madawati hayo
Walimu wa shule ya msingi Misasa wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la
mkuranga Abdallah Ulega mara baada ya kuzuru shuleni hapo kwa lengo la
kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii na kwamba yeye kama kiongozi wao yupo
pamoja nao .
Akina mama wa kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Likanga
wakimsilikiliza mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwa makini wakati
akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru uliofanyika kijiji hapo
ambapo pia walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zao hususani kukosekana
kwa Zahanati na maji safi.
..............................................................................................................................................
Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi madawati 537 kwa
halmashauri ya wilaya hiyo, huku akiwataka viongozi wakiwamo madiwani wa kata
mbalimbali kusimamia vizuri madawati hayo ili kutambua mchango mkubwa wa Rais
Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi alisema kuwa madawati hayo yametokana na fedha zao ambazo zilibaki baada ya kubana matumizi katika ofisi ya bunge na kwa kauli moja walikubali kumkabidhi Rais Dkt. Magufuli, ambapo naye kwa kutambua changamoto ya madawati akaelekeza fedha hizo zipelekwe kutengeneza madawati hayo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msham Munde alimshukuru Mbunge huyo na kudai kuwa uchangiaji wa madawati hayo ni mchakato endelevu hivyo wadau waendelee kujitokeza kuchangia huku akisisitiza kwamba kwa asilimia kubwa yamekwenda kutatua kero hiyo.
Wakati huohuo mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke alimkabidhi mbunge wa jimbo hilo Ulega Madawati 50 kama sehemu ya kumuunga mkono mbunge paoja na Rais Dkt Magufuli huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia ili watoto wasome katika mazingira rafiki.

No comments:
Post a Comment