Pichani kati ni Mratibu wa tamasha la Dar Festival, Faridi Faraji
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar es Salaam juu ya
tamasha hilo litakalofanyika mwezi huu katika viwanja vya
viwanja vya leaders club na siku ya pili ndani ya viwanja vya Makumbusho jijini
Dar.Kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala na kushoto ni mmoja wa Waratibu wa
tamasha hilo, Shaban Kapilima.
.................................................................................................
Na Sara Zuberi
Mratibu wa Tamasha la Dar Festival, Faridi Faraji amesema kuwa tamasha hilo jipya litalenga kutangaza
na kudumisha utamaduni wa Tanzania,na kuwa tamasha hilo litahusisha michezo ya
kiasili kama Bao,Karata ambalo litaenda sambamba na burudani nyingine za ngoma
za asili na maonesho ya baadhi ya tamaduni za makabila ya Tanzania.
" Pia tunategemea kuwa na
mashindano ya kucheza ,vichekezo na maonyesho ya Muziki kutoka kwa baadhi ya
Wasanii" alisema Faridi.
Amesema kuwa kutokana na
utafiti inaonyesha watu wengi wamekuwa wakikosa matukio kama haya na, hivyo
wanatarajia tamasha hilo litapokelewa kwa furaha kubwa na Watanzania
watajitokeza kwa wingi kwani litahusisha watu wa rika mbalimbali.
Akifafanua zaidi faida ya
tamasha hilo, Faridi amesema kuwa tamasha hilo litaendeleza umoja wa
Watanzania, Burudani kwa Watanzania, kuwakumbusha Watanzania utamaduni wao, kutangaza
utamaduni wa Watanzania samnbamba na kusaidia Serikali kupitia sekta ya utalii
ili kuongeza pato la taifa.
Faridi ametoa wito kwa
wanahabari kulitangaza tamasha hilo ili wadau wajitokeza kwa kulidhamini,hivyo
kwa pamoja watakuwa wamesaidia kudumisha utamaduni wetu na kuisaidia
serikali yetu kutunza utalii.
No comments:
Post a Comment