Madereva wanaofanya safari kutoka Bagamoyo kwenda
Dar es Salaam, leo wamegoma kutoa huduma hiyo ili kuishinikiza Halmashauri ya
Bagamoyo kupunguza Ushuru unaotozwa katika kituo cha mabasi Bagamoyo ambao ni
shilingi 2000 kutoka shilingi 500 ya zamani.
Akizungumzia swala hilo makamo Mwenyekiti wa
Umoja wa Madereva Dar Bagamoyo, Hassani Manamba, alisema madereva
wamefikia uamuzi huo kutokana na kiwango
cha ushuru kuwa kikubwa kinachotozwa
kila gari inapotoka kituoni.
Alisema Halmashauri imebandika Tangazo la
kubadilisha bei hiyo bila ya kuwashirikisha wahusika ambao ni madereva, ili kukubaliana
au kutokubaliana na bei hiyo mpya.
Nae Makamo Mwenyekiti wa Sakosi wa umoaja wa
Madereva, Manja Diksoni Mwaibula, alisema swala la kupandisha ushuru katika
kituo cha mabasi Bagamoyo
halikushirikisha wadau wa usafirishaji jambo ambalo limeleta usumbufu katika
utekelezaji wake.
Alisema awali malipo yalikuwa shilingi mia tano
kila Gari inapotoka ambapo sasa kila
Gari inatakiwa kulipa shilingi elfu mbili kila inapotoka kituoni jambo ambalo
madereva wameligomea.
Aliongeza kuwa malipo ambayo yapaswa kulipawa
kila Gari inapotoka kituoni ni vigumu kutekelezeka kwakuwa kama gari itatoka
mara nne kwa siku inapaswa kulipa shilingi elfu nane wakati bado hesabu ya
mwenye gari, mafuta nk. "hii
ni kutuwekea mazingira magumu ya kufanya
kazi hii", Alisema.
BAGAMOYO KWANZA BLOG imemtafuta Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy Issah, ambae amekiri kuwepo kwa mabadiliko
hayo na kusisitiza kuwa hiyo ni sheria iliyopitishwa kwenye Baraza la madiwani na kusainiwa na waziri ambapo madereva
walipelekewa Tangazo kwaajili ya
utekelezaji.
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri alisema swala
malipo ya ushuru ni mikakati ya Halmashauri katikia kuongeza pato la ndani na kwamba sheria hiyoimepitishwa kwa mujibu wa
utaratibu ingawa kwenye utekelezaji wa sheria mbalimbali kunakuwa na changamoto
zake.
Kufuatia hali hiyo Mbunge wa jimbo la Bagamoyo,
Dkt. Shukuru Kawambwa, alifika katika
kituo cha mabasi ambapo aliwataka madereva kukutana na uongozi wa
Halmashauri ili kujadili swala hilo na kulipatia ufumbuzi.
Abiria mbalimbali walionekana kuzagaa katika kituo
hicho cha mabasi Bagamoyo bila ya kupata usafiri, ambapo baadhi yao
wamekuwa wakikodi bajaji kwa gharama ya shilingi 5000 kutoka Bagamoyo mpaka Bunju, huku wengi wao wakishindwa kusafiri
na kulazimika kurudi nyumbani.
Wakizungumzia
hali hiyo Abiria katika kituo cha mabasi Bagamoyo wamesema hali hiyo
imewaathiri kiuchumi kwakuwa wengi
wanaosafiri asubuhi wanwahi sehemu zao za kazi ambapo watu wengi leo
wameshindwa kufika maofisini.
Aidha,
wamlisema kuwa, katika hali kama
hiyo serikali pia inapata hasara kwakuwa
haiwezi kupata mapato yake kupitia ushuru kwakuwa Madereva wa magari yote wamegoma jambo am balo litadhoofisha
pia uchumi wa Halmashauri.
Abiria hao wameitaka Halmashauri ya Bagamoyo
kukaa chini na wadau wa Usafirishaji Bagamoyo ili kuona namna ya kutatua tatizo
hilo ili kufikia muafaka utakaoleta manufaa kwa pande zote tatu, kwa maana ya Madereva, Halmashauri
na Abiria.
Makamo mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Dar. Bagamoyo, Hassani Manamba, akimueleza Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, hayupo pichani, sababu iliyowafanya wagome.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, akiwasikiliza madereva katika kituo cha mabasi Bagamoyo, leo baagda ya Madereva hao kugomea ushuru wa shilingi 2000 kwa kila Gari inapotoka getini bada la ya shilingi 500 ya awali.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawmbwa akizungumza na madereva wa kituo cha mabasi Bagamoyo ambao wamegoma kutoa huduma usafiri kutoka Bagamoyo kwenda Makumbusho Dar es Salaam.
Dereva wa Basi la Bagamoyo Dar. Mr. Ngomuo, akielezea kilichopelekea kugoma.
No comments:
Post a Comment