Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa-NIDA- Dickson
Maimu (wa tatu kushoto) na viongozi wengine nane wa taasisi hiyo
wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mapema hii leo.
..................................................................................
..................................................................................
Mnamo mwezi January 2016, Rais Dkt. Magufuli aliamua kutengua uteuzi wa
Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) Bwana Dickson Maimu na
kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine ili kupisha uchunguzi wa namna
ilivyotumika kiasi cha shilingi bilioni 179.6
Katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa malamiko mengi yamepatikana ikiwa ni pamoja na
kuchelewa kupatikana vitambulisho hivyo huku maeneo mengi yakiwa wananchi
hawajapata mpaka sasa.
Katika kutengua uteuzi wa
Mkurugenzi huyo wa NIDA Dickson Maimu, Rais Dkt. Magufuli aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
nchini (TAKUKURU) ifanye uchunguzi wa namna
fedha hizo zilivyotumika na ikiwa kunavitendo vya rushwa hatua za kisheria
zilchukuliwe dhidi ya wahusika.
Aidha, alizitaka pia Taasisi za
Ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) na ile ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika
Sekta ya Umma (PPRA) ilitakiwa
kufanya uchunguzi wa manunuzi yote
yaliyofanywa na NIDA.
Katika uchunguzi huo Ofisi ya mkaguzi mkuu wa
hesabu za serikali CAG, ilitakiwa kufanya uchunguzi na kuangali vitambulisho
vya taifa kama vinaendana na kiasi cha fedha zilizotumika na NIDA ambazo ni
bilioni 179.6
No comments:
Post a Comment