Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Good News
For All, Askofu Dkt. Charles Gadi akifanya maombi mara baada ya kuongea
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo
jijini Dar es Salaam.
Askofu
Dr. Charles Gadi akiongea na wanahahabari hawapo pichani kuhusu mkutano wa
maombi ya kitaifa wa kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk.
John Pombe Magufuli. maombi hayo yatafanyika geita hivi karibuni
......................................................................................................
Askofu Dkt Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono Rais John
Magufuli,katika mchakato wake wa kuamishia serikali makao Makuu ya nchi Mkoani
Dodoma kwani ni uamuzi wa kijasiri na upaswa kuungwa mkono.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dare Es Salaam Askofu Gadi amesema
kuwa jitihada zinazofanywa na Rais magufuli ni kubwa kwani jitahada zinaonekana
wazi za kuimarisha mji wa Dodoma na ili uweze kutumika kama makao makuu ya
nchi.
‘’Serikali inafanya kazi nzuri kinachotakiwa ni kumtia moyo Rias wetu ili
jambo ili lifanikiwe na kuhamisha serikali ili kutimiza mpango wa muda mrefu wa
kuhamisha serikali kutoka Dar es Salaam na kwenda Dodoma’’alifafanua askofu
Gadi
Aidha amesema Serikali imejipanga na inaandaa mazingira mazuri kwa
watumishi wake watakao hamia huko kupata mahitaji yote muhimu wanayohitaji,na
kuongeza kuwa jambo hilo litaharakisha maendeleo katika mikoa jirani na Dodoma.
Ameongeza kuwa imekua ni kawaida ya baadhi ya watu kulalamika kila
linapotokea jambo bila kusikiliza na kufatilia jambo hilo kwa makini,amewaomba
watanzania wasiwe watu wakulalamika kulaumu na badala yake wawe watu wakusiliza
na kufata maelekezo.
Ameongezea kuwa watafanya maombi ya kumuombea Rais John Magufuli na
viongozi wa serikali katika mji wa buselesele wilaya ya chato mkoani Geita
agosti 25 mwaka huu,kuombea mvua,amani,upendo na mshikamano baina ya serikali
na wananchi wake.
‘’Maombi haya ni ya kumuomba Mungu alifanye taifa letu kuwa taifa
bora kwa uchumi,astawi wa watuwake na linaloongoza kwa amani na mafanikio
katika kila sekta ‘’alifafanua Askofu Gadi.
No comments:
Post a Comment