Amina Diahunga, ambae ni mlemavu wa miguu akimueleza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo namna alivyoteswana wafugaji jamii ya kimasai wakati mkuu wa wilaya alipotembelea kata ya Miono hivi karibuni. |
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga
ametoa amri ya kukamatwa wale wote waliompiga na kumnyanyasa mama mwenye ulemavu wa miguu, Amina Diahunga akiwa
shambani kwake Kitongoji cha Umasaini kata ya Miono.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo mbele ya
mkutano wa Hadhara uliofanyika hivi karibuni kata ya miono, ambapo alisema
hata kama wamekimbia watafutwe na
wafunguliwe mashtaka.
Mkuu wa wilaya ametoa kauli hiyo kufuatia
malalamiko aliyoyatoa mama huyo ya
kwamba wafugaji jamii yakimasai wanamnyayasa kwa
ulemavu wake kwa kitendo cha kuingiza mifugo kwenye shamba lake na kumpiga.
Mama huyo alimwamiba mkuu wa wilaya kuwa lkicha
ya ulemavu wake hapendi kupita barabarani kuomba na hulazimika kulima kwa jembe
la mkono huku akiwa amekaa ambapo anaweza kupata chakula kwa mahitaji yake.
Aliendelea kusema kuwa pamoja na juhudi hizo
anazozifanya bila ya kuwa na msaada
wowote, wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao na kuharibu mazao yake na
anapojaribu kuwakemea wanampiga bila ya kupata msaada.
''Walinipiga
mpaka wameniumiza lakini sikupata
wakunitetea nifanyeje naomba msaada wako mkuu wa wilaya'',
Alisema mama huyo kwa uchungu.
Mkuu wa
wilaya alimuagiza mkuu wa polisi wilaya
ya Kipolisi Chalinze, kuhakikisha anawakamata wote waliohusika na kumnyanyasa mama huyo.
Aidha, aliongeza kuwa hata kama muda umepita
waliofanya tukio hilo watafutwe na wakipatikana walipe fidia ya mazao na
kufunguliwa mashtaka.
Siwezi
kuvumilia unyanyasaji huu lazima watafutwe, wakamatwe na wafunguliwe mashtaka
na walipe fidia ya mazao ya huyu mama, Alisema mkuu wa
wilaya.
Kitongoji cha Umasaini kata ya Miono ni eneo linalokaliwa
na wafugaji na wakulima ambapo katika mpango wa matumizi bora ya Ardhi, serikali ya kijiji imetenga maeneo kwaajili ya
wafugaji na wakulima ili kuondoa
migogoro ya mara kwa mara.
Hata hivyo
licha ya kuwepo kwa mpango wa matumizi bora ya Ardhi, wamekuwa wakitaka kukaana
mifugo yao katika eneo lililotengwa
kwaajili ya makazi hali inayoleta mgogoro miongoni mwa wakazzi.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid hemed mwanga
alifika maeneo yaliyotengwa na mpango wa
matumizi bora ya Ardhi ambapo alikuta
mgogoro kati ya wafugaji na wakulima.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya
Bagamoyo aliwataka wafugaji kuheshimu mpango na kwamba wale wote walioingia
kwenye mashamba wa wakulima watoke mara moja.
Wkazi wa kitongoji cha Umasaini wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed mwanga mara alipotembelea eneo hilo kusikiliza malalamikoa yaliyopo kati ya wakulima na wafugaji. |
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Umasini kata ya Miono. |
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Umasaini aliyevaa Jaketi na T.shet nyekundu, Rashidi Litibi, akimuonesha mkuu wa wilaya kibao kinachoelezea mpango wa matumizi bora ya Ardhi. |
Wananchi wa kata ya Miono wilayani Bagamoyo, wakiwa makini kumsikiliza mkuu wa wilaya hiyo, hayupo pichani. |
No comments:
Post a Comment