Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina wa Polisi, (Deputy Commissioner of Police-DCP.)
Mohamed Mpinga, akizungumza na wamiliki wa shule za udereva (hawapo
pichani), wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za
Udereva Tanzania (Chashubuta), Hoteli ya Dreamers Buguruni Dar es Salaam leo.
...............................................................................................................
JESHI la Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya
udereva nchini ambavyo havina sifa.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP)
Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za
Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
"Kuanzia sasa Jeshi la Polisi
halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva kitakachokosa sifa kwani kwa
kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali na hivyo kuongeza vifo na
majeruhi" alisema Mpinga.
Mpinga alisema kwa mujibu
wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E 2002) mpaka sasa jeshi la
polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo zitategemewa kutoa madereva bora
wenye kuzingatiasheria za usalama barabarani kuepuka ajali za mara kwa mara
zinazosababishwa na madereva wasiokuwa
na taaluma.
Alisema jeshi hilo
litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havina sifa na wamiliki wake
kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kuvifungia vyuo hivyo.
Awaliakisoma risala mbele
ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla alisema Chama
hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wadau wa sekta ya
usafiri na usafirishaji kutothamini mchango mkubwa unaotolewa na shule za
udereva za watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya
serikali pekee.
Mkolla alimuomba Kamanda
Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili iende sanjali na mahitaji ya
barabara, vyombo na wakati, huku akimuba
shule hizo ziwe zinashirikishwa katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala
hiyo.
Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla (katikati),
akimkabidhi risala yao Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina
wa Polisi, (Deputy
Commissioner of Police-DCP)
Mohamed Mpinga, Kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi,(Assistant Superintendent
of Police- ASP.) Deus Sokoni.
Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Msaidizi
wa Polisi, (Assistant Superintendent
of Police- ASP.) Deus Sokoni (kulia), akifafanua baadhi ya vifungu vya sheria
katika mkutano huo.
Picha ya pamoja mgeni rasmi na wamiliki wa shule za udereva nchini
waliohudhuria mkutano huo.
No comments:
Post a Comment