Saturday, August 27, 2016

DC BAGAMOYO AONGOZA ZOEZI LA USAFI KWA KUENDESHA TREKATA LA KUBEBEA TAKA

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed  Mwanga, akiongoza zoezi la usafi kwa kuendesha Trekta  la kubebea taka.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu Mwandamizi wa  Polisi, SSP-Adam Maro, kulia akishiriki kufanya usafi katika mji  wa Bagamoyo leo asubui, kushoto ni  Sajenti, SGT-Piyusi akiendelea  na zoezi la  usafi.

Mkuu wa Gereza  la Kigongoni, Superintendent- Muyengi Machum Bulilo, akifanya usafi katika mitaa ya Bagamoyo, ikiwa ni siku ya kufanya usafi kwa pamoja

Jeshi la polisi,  Jeshi la Magereza wakishiriki vyema katika zoezi  la usafi katika mitaa ya Bagamoyo, kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya Bagamoyo, Mrakibu Mwandamizi wa  Polisi, SSP-Adam Maro, na kushoto anaefagia ni mkuu wa Gereza  la Kigongoni Bagamoyo,  Superintendent- Muyengi Machum Bulilo.

Kikosi cha askari magereza Bagamoyo wakiwa kwenye zoezi la usafi.

Wafanyakazi wa DAWASA, wakiwa katika zoezi la usafi mjini Bagamoyo.

Wafanyakazi wa DAWASA, wakiwa katika zoezi la usafi mjini Bagamoyo.
Mkuu wa idara ya utumishi Halmashauri ya Bagamoyo, Grace Mbilinyi, mwenye fulana nyeusi kushoto akishiriki zoezi la usafi leo  jumamosi katika mji wa Bagamoyo, wenye  fulana  nyeupe ni wafanyakazi wa DAWASA, kulia mwenye fulana nyekundu ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi, A/INSP Rose.

Mkuu wa idara ya utumishi Halmashauri ya Bagamoyo, Grace Mbilinyi, mwenye fulana nyeusi kushoto akishiriki zoezi la usafi leo  jumamosi katika mji wa Bagamoyo, kulia ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi, A/INSP Rose.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga akipanda kwenye Trekta tayari kwaajili ya kubeba taka zilizokusanywa, kulia mwenye miwani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Daktari, Amiri Ibrahim Batenga wakati wa zoezi lausafi lililofanyika  kwa pamoja leo jumamosi katika mji wa Bagamoyo.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya Bagamoyo, Daktari, Amiri Batenga mwenye miwani katikati akifurahia jambo na Mkuu wa Idara ya Utumishi Halmashauri ya Bagamoyo Grace Mbilinyi kushoto, na kulia ni Diwani wa viti maalum magomeni, Shumina Rashidi, wakiwa tayari wamepakia  taka kwenye Trekta  ambalo linaonekana kwa mbali likiendeshwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga.


Diwani wa kata ya Magomeni, Mwanaharusi Jarufu, kushoto akipakia taka kwenye Toroli katika zoezi la usafi  lililotekeleza  leo mjini  Bagamoyo  amb ali limeongozwa na mkuu wa wilaya ya bagamoyo, Majid Hemed mwanga.


Mkuu wa idara ya  utumishi  Halmashauri  ya Bagamoyo, GraceMbilinyi, mwenye fulana nyeusi akiwa katika harakati za usafi uliofanyika  kwa  pamoja  leo mjini Bagamoyo ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Pwani, Hance John Mwankenja, aliyesimama kushoto akiwa pamoja na wananchi mbalimbali katika zoezi  la usafi mjini Bagamoyo.


Wananchi mbalimbali katika mji wa  Bagamoyo wakishiriki zoezi la usafi wa mazingira wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,  Majid  mwanga.



Wananchi  wakishirikiana  vyema  kabisa na jeshi  la magereza na wadau  wengine katika usafi  wa mazingira hapa ni Stendi ya Kongoa Bagamoyo.


Jeshi la Polisi, Jeshi  la Magereza, na wafanyakazi wa NMB wakiwa katika harakatiza usafi katika mji wa Bagamoyo uliofanyika  leo jumamosi  tarehe 27-08-2016.

No comments:

Post a Comment