Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Shaka Hamdu Shaka akiwaonesha Waandishi wa habari barua walioiandikia Jeshi la
Polisi kuomba kibali na Ulinzi cha kufanya Maandamano hayo ya
amani,wanayotarajia kufanya Agosti 31,kwa lengo la kumpongeza na kueleza
Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Shaka Hamdu Shaka akitoa ufafanuzi kwa baadho ya maswali mbalimbali yaliyokuwa
yakiulizwa na Waandishi wa habari kuhusiana na Maandamano hayo ya amani
yanayotarajiwa kufanyika Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na kueleza
Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa habari Makao makuu ya Ofisi hizo
mapema leo jijini Dar kuhusiana na kufanya maandamano ya amani Agosti 31,kwa
minajili ya kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe
Magufuli.
.................................................................................................................
Umoja wa Vijana wa Chama
cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani Agosti 31 kwa
ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.
Akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu
Shaka amesema kuwa maandamano hayo wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la
Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo’
Amesema kuwa wasipopata
ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa
wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.Shaka amesema
kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na
maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha amesema kuwa
maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja
tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment