Muonekano wa Uwanja wa Uhuru
mara baada ya matengenezo.
Picha zote na Raymond
Mushumbusi WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya
Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22,2016 .
........................................................................................
Vyama vya michezo nchini vimeshauriwa kujenga ofisi zao ndani ya uwanja
wa Uhuru kuepukana na gharama za kukodi ofisi katika maeneo mengine.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye wakati akipokea Uwanja wa
Uhuru uliokuwa unafanyiwa matengenezo na kampuni ya CBG.
Mhe. Nape Moses Nnauye amesema kuwa mpaka sasa michoro kwa ajili ya
majengo ndani ya Uwanja huo ipo tayari na vyama vya michezo vinakaribishwa
kuanza kujenga ofisi zao.
“Kama kuna vyama vya michezo vyenye uwezo binafsi au kama wanaweza kupata
ufadhili wa kuja kujenga ofisi zao humu michoro ipo tayari na eneo lipo tayari
ata kesho waje wajenge ” alisema Mhe. Nape.
Mhe. Nape amesisitiza kuwa zoezi hili litaratibiwa na Serikali moja kwa
moja na kutoa nafasi kwa vyama vyenye uwezo kujitokeza na kuchangamkia fursa
hiyo ambapo ramani,michoro na eneo lipo tayari kwa ajili ya zoezi hilo.
Aidha Serikali imewaalika wadau mbalimbali kuwekeza katika michezo kwa
kujenga miundombinu itakayosaidia kukuza vipaji kwa wanamichezo mbalimbali na
kusukuma gurudumu la maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof Elisante Ole Gabriel amevishauri vyama vya michezo nchini
kuchangamkia fursa iliyotolewa na Serikali ya kujenga ofisi za vyama vyao ndani
ya Uwanja wa Uhuru na kushauri wadau wa michezo kuwekeza zaidi katika michezo
hasa kwa vijana.
“ Wadau kimbilieni fursa ndio hii ya kuwekeza katika michezo pamoja na
vyama vya michezo kujenga ofisi zao ndani ya Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya
maendeleo yao na michezo nchini” alisema Prof Gabriel.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongozana na
baadhi ya viongozi wa Wizara na Uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili katika
makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo 22 Agosti 2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye akiangalia nyasi za Uwanja wa Uhuru mara baada ya kukabidhiwa
uwanaja huo baada ya matengenezo leo Agosti 22,2016.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(kulia) akibadilishana hati za makabidhiano ya
Uwanja wa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa matengenezo leo Agosti 22,2016.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole
Gabriel(kulia) akionesha hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru kwa
waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa matengenezo ya uwanja huo leo
Agosti 22,2016 (katikati ) ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa michezo mara
baada ya makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22,2016.
No comments:
Post a Comment