Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali Bungeni leo
tarehe 15 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Omary Mgumba (Mb) akifuatilia mkutano wa kumi
na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili 2019.
Mwingine pichani ni Naibu Waziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe
Juliana Shonza (Mb).
......................................
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali inayo dhamira ya kukamilisha skimu zote za umwagiliaji ambazo utekelezaji wake haujakamilika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Azza
Hillal Hamad aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji katika Kijiji cha Ishololo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mhe Mgumba amesema kuwa Skimu hiyo ipo miongoni mwa skimu za umwagiliaji
zitakazopewa kipaumbele katika kutekeleza Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji (Irrigation Master Plan 2018 – 2025) ambao kwa sasa umeanza kutekelezwa.
Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo mradi wa umwagiliaji Ishololo,
tayari
Serikali imekwishaanza mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA kwa lengo la kuboresha miradi yote ambayo haijakamilika na ile inayofanya kazi chini ya ufanisi uliokusudiwa.

Naibu Waziri huyo wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa wa Ishololo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini ni moja kati ya miradi iliyokuwa ikitekelezwa kupitia Mradi wa Uwekezaji katika
Kilimo katika Wilaya (DASIP) chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Kilimo katika Wilaya (DASIP) chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Alisema Utekelezaji wa Mradi huo ulifikia ukomo wake mwezi Desemba 2013 ambapo Benki
Maendeleo
ya Afrika ilisitisha kutoa fedha za utekelezaji wa miradi wakati utekelezaji wake ukiwa haujakamilika.
ya Afrika ilisitisha kutoa fedha za utekelezaji wa miradi wakati utekelezaji wake ukiwa haujakamilika.
No comments:
Post a Comment