Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akiwa katika ofisi mpya za wizara hiyo katika mji wa serikali Ihumwa jijini Dodoma.
............................................
Wizara ya Nishati imetekeleza agizo
la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, alilotoa mwishoni mwa wiki iliyopita
kuwa viongozi wote wa Wizara wahamie katika mji wa serikali Ihumwa jijini
Dodoma.
Tayari viongozi wote wakuu wa wizara hiyo ambao ni
Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu wamehamia Ihumwa tangu Jumatatu ya Aprili
15, 2019 ambapo wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.
Aidha, zoezi la viongozi wengine
pamoja na watumishi wa Wizara hiyo kuhamia Ihumwa linaendelea ambapo wasaidizi wa
viongozi hao wakiwemo masekretari, madereva na wahudumu wamekwishahamia pia.
Katika zoezi hilo linaloratibiwa na
Idara ya Utawala, linahusisha kuweka vitendea kazi katika ofisi mbalimbali
zilizosalia na kuhamisha watumishi waliosalia.
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na watumishi wa wizara hiyo mara alipowasili katika jengo jipya la wizara ya Nishati
Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu akiwa katika lango kuu la kuingilia ofisi za wizara hiyo jijini Dodoma
Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Hamisi Mgalu, akiwa ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kuhamia rasmi kwenye jengo jipya la wizara hiyo tayari kwa utekelezaji wa majukumu ya Taifa.
Watumishi wa Waziri
wa Nishati, wakiangalia mabox ambayo ndani yake kuna vifaa kwaajili ya matumizi ya ofisi hiyo vikiwa bado havijapangwa kwenye utaratibu wake unaotakiwa wakati wizara hiyo ilipohamia rasmi katika jengo lake jipya jijini Dodoma.
Watumishi wa Waziri
wa Nishati, wakiwa na nyuso za furaha baada ya kuingia kwenye jengo jipya la wizara hiyo katika mji wa serikali Ihumwa jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment