Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Makampuni ya Simu
nchini, itawezesha zoezi la uandikishaji wa watumiaji wa simu nchini kwa
kutumia Namba za Utambulisho wa Taifa au Kitambulisho cha Taifa. Zoezi la
Uandikishaji wa laini za simu linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 01-Mei-2019.
Mazoezi ya majaribio ya zoezi hili yamefanyika katika baadhi ya Mikoa na
Taasisi na kuonyesha mafanikio.
NIDA tayari imesajili asilimia 88 ya watu wote
wanaostahili kusajiliwa kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa nchi nzima.
Zoezi
la Utambuzi na usajili ni endelevu, hivyo asilimia 12 ya lengo la usajili
lililobaki linaendelea kutekelezwa katika wilaya zote nchini kwa kusajili watu
ambao hawakusajiliwa kwenye zoezi la usajili wa umma (Mass Registration) na
ambao wamekisha umri wa miaka 18, ambacho ni kigezo cha kisheria kinachoruhusu
mwananchi kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa.
Vile vile usajili
wa umma unafanywa tena katika mikoa ambayo watu wengi hawakusajiliwa katika usajili
wa awali. Mikoa hiyo ni pamoja na Dar es salaam, Tanga, Pwani na Kigoma.
NIDA tayari imetengeneza Namba za Utambulisho wa
Taifa Milioni 12, sawa na asilimia na 59 ya usajili uliofanyika. Zoezi la
uhakiki, kuchakata na kutengeneza Namba za Utambulisho wa Taifa linaendelea
kutekelezwa kwa kasi usiku na mchana.
Aidha tunatoa rai kwa wale wote ambao
wamejulishwa kuwa vitambulisho vyao vipo tayari wafike Ofisi za NIDA au Ofisi
za Serikali za Mitaa walipo jiandikishia kuvichukua. Vitambulisho vya Taifa vinaendelea
kuzalishwa na kusambazwa kwa wananchi.
Namba za Utambulisho wa Taifa zitatumika
katika usajili wa Namba za simu na matumizi mengine. Hivyo wale ambao tayari
wana Namba za Utambulisho wa Taifa wazitumie kujisajili wakati vitambulisho
vinazalishwa.
Wananchi mnaweza kupata Namba ya Utambulisho wa
Taifa na huduma zingine zitolewazo na NIDA kwa njia zifuatazo:-
a. Kupiga namba * 152 *00#; chagua Ajira na
Utambuzi; Chagua NIDA
b. Kupakua nakala ya Kitambulisho cha Taifa kwa
kutembelea tovuti: https://services.nida.go.tz/nidportal/NID_Copy.aspx au
tovuti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.
c. Kupiga simu huduma wateja; 0673 333444, 0743
202020, 0743 201020,
d. 0759 102010, 0765 201020.
e. Kufika ofisi za NIDA ya Wilaya ilyopo karibu.
Ni Muhimu kwa Wananchi wote wenye sifa za
kusajiliwa kwa ajili ya Utambulisho wa Taifa kufanya hivyo sasa pasipo kusubiri
mpaka wanapokuwa na hitaji la haraka kwani uhakiki wa taarifa zako lazima
ufanyike kabla ya utoaji wa Namba ya Utambulisho wa Taifa na baadae
kitambulisho cha Taifa.
“Utambulisho wa Taifa kwa Maendeleo na Ustawi wa
Nchi Yetu”
Imetolewa na
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
23 APRILI, 2019.
No comments:
Post a Comment