NA
MWAMVUA MWINYI, Mafia
MBUNGE
wa viti maalum Mkoa wa Pwani ,Zaynabu Vullu, ametoa kitanda na vifaa tiba
katika zahanati ya Kijiji cha Malimbani ,wilayani Mafia.
Aidha
mbunge wa Jimbo la Mafia Mbaraka Dau nae amekabidhi mashine ya kusambazia maji,
kata ya Kiegeani ili kuwarahishia wakazi hao kupata huduma hiyo kupitia kisima
kilichochimbwa eneo hilo.
Vullu
alikabidhi vifaa hivyo ,wakati alipokuwa kwenye ziara ya siku mbili wilayani
Mafia, kwa lengo la kutimiza ahadi yake ya kukabidhi vifaa hivyo vinavyolenga
kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wakazi hao, ambapo alipokelewa na mwenyeji
wake Dau.
Alisema
, anaunga mkono juhudi za serikali kwa kununua kitanda, na vifaa tiba
vitavyosaidia wagonjwa wataokwenda kupatiwa huduma kwenye zahanati hiyo
“Niwapongeze
kwa umoja, upendo na mshikamano ambao mnaendelea kuuonyesha katika kujiletea
maendeleo, nami leo nimekuja kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuelekeza
nguvu katika kuboresha sekta ya afya” alisema Zaynab.
Nae
Dau alielezea kwamba ,amenunua mashine hiyo inayolenga kuboresha upatikanaji wa
maji katika kisima kilichopo, ambacho kwa sasa ni cha mdundiko.
Alielezea,
baada ya kufungwa mashine maji yatakuwa yanasambazwa umbali wa mita
1,000. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwajupi Abdallah Sharifu aliwashukuru
wabunge hao kwa namna walivyojitoa katika sekta hizo.
No comments:
Post a Comment