Kamati ya Amani Mkoa wa Pwani imetembelea eneo la Mradi wa Umeme wa mto Rufiji na kufanya maombi maalum ili utekelezaji wake ukamilike kwa ufanisi na kwa wakati uliopangwa.
Kamati hiyo yenye wajumbe kutoka
madhehebu mbalimbali imeshiriki kwenye ziara ya siku tatu iliyoanza April tisa
ikijumuisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani na ya
Wilaya ya Rufiji, Wakuu wa Wilaya sita, Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Rufiji pamoja na Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha
Mloka.
Wakiwa katika eneo la mradi, msafara
huo ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo ulipokea
maelezo ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati kutoka kwa Wataalamu wa
Shirika la Umeme nchini-TANESCO wanaosimamia mradi huo.
Akifafanua lengo la ziara hiyo, Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo alieleza kuwa sehemu ya eneo la
ujenzi wa mradi liko katika Mkoa wa Pwani hivyo ni wajibu wa jamii kuwa na
uelewa mpana na wajibu wa kushiriki katika utekelezaji na kulinda miundombinu
yake ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zilizopo au zinazoweza kujitokeza na
kuzipatia ufumbuzi.
“Asilimia kubwa ya shughuli za
utekelezaji wa mradi huu zitakuwa katika eneo la Mkoa wa Pwani hivyo tunataka
tuone namna ambavyo Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Amami
itashughulikia maswala yote yaliyoko ili mradi huu usikwame” amesema Mhandisi
Ndikilo.
Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa pamoja na
kuwa wataalamu wa kitanzania na Mkandarasi wako kwenye eneo la utekelezaji
wakiendelea na majukumu yao, bado kuna mambo mengine nje ya eneo hilo ambayo
Mkoa kwa kushirikiana na Taasisi nyingine zinawajibu wa kuyasimamia ili
kuhakikisha kuwa utekelezaji unafanikiwa na kwa wakati
No comments:
Post a Comment