Na Selemani Magali
Rais
mstafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewataka jamii, walezi na
wadau kuwapenda, kuwajali na kuwathamini watoto wenye ugonjwa wa usonji,
akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwapa furaha.
Dkt
Kikwete amesema watoto wenye matatizo ya usonji (Autism) wapo sawa na watoto
wengine kinahitajika ni malezi yenye upendo kutoka kwa jamii ili nao wajihisi
wako sawa na watoto wengine hapa Nchini.
Dkt
Kikwete ametoakauli hiyo mapema hii leo wakati akizungumza katika viwanja vya
shule ya AL-MUNTAZIR baada ya matembezi kwa ajili ya kueneza uelewa kwa jamii
kuhusu umuhimu wa kuwapenda watoto wenye ugonjwa wa usonji kwani nao ni watu
kama wengine ambao wanaweza pewa fursa ya kushiriki kwenye shughuli
mbalimbali za kijamii.
Watoto
wenye hali ya usonji wana shida katika kuwasiliana na tabia zao ni kurudia
rudia mambo anayofanya mara kwa mara na pia watuwengi wenye ugonjwa huu
wananamna yao ya kujifunza, kusikiliza na kuitika.
“Mfano
wa hali hii ni kwamba katika hali ya kawaida, mtoto wa mwaka mmoja hutabasamu
au kuwa na furaha kila wakati, huiga mambo mbalimbali anayoona na kufuatilia
vitu anavyoviona vikisogea, lakini mtoto mwenye ugonjwa huu hafanyi vitu hivi.
Wadau
wanasema Kukosa uelewa wa hali hii ya watoto wenye mahitaji huwafanya walimu na
wazazi kudhani watoto ni watundu, wavivu au wanakera na wakati mwingine
huadhibiwa kwa sababu hiyo wakati kwamba watoto hawa wanahitaji uangalizi wa
karibu, kupendwa na kupata msaada kutoka kwa walimu na wenzao.
No comments:
Post a Comment