NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
MTU
mmoja amefaliki Dunia na wengine wawili kujeruiwa baada ya kulipukiwa na Mtungi
wa kuchemshia Korosho katika mafunzo ya ubanguaji bora wa korosho yanayotolewa
na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Lindi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Katibu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa Mkoani Lindi Sokoine
Bonifas Lymo amekili kupokea majeruhi wawili Amadeo urio lio (27) ambae ni
mwanajeshi wa jeshi la kujenga Taifa JKT kambi ya Nachingwe Mkoani Lindi na
mwingine ni Asha Ahmedi (30) Mkazi wa Njangao Halmashauri ya wilaya ya Lindi na
Maiti moja ya Saada Juma (28) mkazi wa kata ya Msinjahili Manispaa ya Lindi
Mkoani humo
Hata
hivyo alisema mpaka sasa majeruhi hao wamepatiwa matibabu na wanaendelea vizuri
ambapo mmoja wa majeruji hao Asha Ahmedi ambae alipata majeraha ya jicho la
kulia baada ya kufanyiwa uchunguzi alionekana hakupata majeraha makubwa
ametibiwa na kurudi nyumbani kwao huku mwingine ambae ni Amadeo Urio lio
alionekana amepata majeraha makubwa mapajani na miguu yote miwili pamoja na
tumboni akiendelea kupatiwa matibabu katika hoapitali hiyo
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Ramadhani
Zungu Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 11, 2019 majira ya saa tano na
nusu Asubuh wakiwa wanaendelea na mafunzo ya ubanguaji wa korosho
"haya
mafunzo tulianza toka jumanne ya Aprili 9 lakini kwa siku ya leo tulikuwa
tumefikia hatua ya kuchemsha , sasa kuna mashine ambayo inatumika kuchemshia
korosho hizo ambapo huchemshwa kwa kutumia mvuke Baada ya kuchochea kuni
joto lilipanda wakati ule wenzetu walikuwa wanajiandaa kuruhusu mvuke kuingia
kwenye korosho Saada ndie aliekuwa karibu na ule mtungi wa kuchemshia Korosho
na Amadeo alikuwa mbali kidogo huku washiriki wengine tukiwa tunaendelea na
mambo mengine"
"
kabla hata hawajaruhusu ule mvuke kutoka na kuingia kwenye Korosho Mtungi ukawa
umelipuka ghafla baada ya kulipuka tukaona yale mabati yake yameenda umbali
fulani tukawasogelea wenzetu tukamkuta Amadeo anatembea na kulia kwa sauti na
Saada akiwa amelala chini ajiwezi " alisema Zungu
Akizungumza
na Waandishi wa Habari baada ya kutembelea eneo la Ajali hiyo Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Lindi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Pudensiana protas
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili
11, 2019 majira ya Saa tano asubuhi katika moja ya majengo ya Shirika
hilo la SIDO huku akieleza kuwa Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
Mtungi wa kuchemshia Korosho ulioripuka kama unavyoonekana pichani.
Mmoja majeruhi katika ajali hiyo akiwa Hospitali ya Rufaa Mkoani Lindi
No comments:
Post a Comment