NA
MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
JESHI
la polisi mkoani Pwani linamshikilia Robison Enerst (33) fundi ujenzi kwa kosa
la kumnyonga shingo, hadi kufa mwanae Modesta Robison mwenye umri wa miezi sita,
akidai sio mtoto wake.
Kamanda
wa polisi mkoani hapo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Wankyo Nyigesa, alieleza kwamba, tukio hilo limetokea
april mosi, mwaka huu huko mtaa wa Vitendo kata ya Misugusugu, Kibaha.
“Kabla
ya kuolewa na mtuhumiwa, mama wa mtoto (marehemu) alikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mwanaume mwingine ambae mtuhumiwa anamtuhumu ndio baba halali wa
mtoto “
“Hali
hiyo ilisababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wazazi hao “alifafanua
Wankyo.
Wankyo
alibainisha, wamemkamata mtuhumiwa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria na
mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, kabla ya
kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.
Kamanda
huyo alitoa rai kwa wananchi, kuwa wanapokuwa na mashaka na jambo fulani la
kihalifu watoe taarifa mapema katika vituo vya polisi ili yaweze kushughulikiwa
mara moja kabla ya kuleta madhara yeyote kwa lengo la kudhibiti
watuhumiwa.
Hata
hivyo, baada ya kumhoji mama wa marehemu yeye alidai mtuhumiwa alishafanya
majaribio ya kumuua marehemu mwanae mara mbili.
Anaeleza,
mara ya kwanza alitaka kumpa sumu ya vidonge lakini mama huyo aliwahi kumuokoa
.
“Mara
ya pili mtuhumiwa alinoa panga ili amkate mtoto lakini hakufanikiwa pia kufikia
april 1, ambapo alimuua mtoto kwa kumnyonga shingo hadi kufariki dunia “
No comments:
Post a Comment