Pichani
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Vulu akizingumza na viongozi wa
Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Mafia mkoani Pwani alipokuwa kwenye ziara ya
siku moja. Meza Kuu wa mwisho kutoka kushoto Arafa Kisela Mjumbe wa Mkoa,
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mafia Mtumwa Geo na Mwenyekiti wa CCM Hassani
Pango.
Picha na Omary Mngindo.
.................................................
Na
Omary Mngindo, Mafia.
WABUNGE
wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu na Subira Mgalu ambaye ni Naibu
Waziri wa Nishati wanataraji kutimiza ahadi walizozitoa wilayani Mafia.
Hayo
yamebainishwa na Vulu alipokuwa kwenye ziara ya siku mbili wilayani hapa,
iliyolenga kukutana na wana- Jumuia zinazounda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo
akiwa Mafia amekabidhi kitanda kimoja kwenye Zahanati ya Maalimbani Kata ya
Kiegeani jimboni hapa.
Akizungumza
na wana-Jumuia ya Wanawake (UWT) wilayani hapa mbele ya Mwenyekiti Mtuma Ahmad,
Katibu Khadija Geo, Mwenyekiti wa CCM Hassani Pango, wa Wazazi Mohamed Fakhi na
Katibu Mashaka Milimila, VULU alisema kuwa wakiwa katika ziara wilayani humo
kuna ahadi ambazo wameziahidi.
"Wana-Jumuia
wenzangu wakati tukiwa kwenye ziara wilayani hapa nikiwa na mbunge mwenzangu
Subira Mgalu kuna mazungumzo mengi ambayo yumezungumza ikiwa ahadi ambazo
tumezitoa ikiwemo viti 100, tunajipanga wakati wowote tutatimiza ahadi
hizo," alisema Vulu.
Aidha
mbunge huyo alipokea taarifa za utekelezaji wa ilani ya chama hicho ikiwemo wa
ugawaji wa taa za sola kwenye zahanati mbalimbali zinazotolewa na Naibu Waziri
Mgalu zinazolenga kuwaboreshea huduma hiyo maeneo hayo.
"Nimepokea
shukrani za mbunge mwenzangu Subira Mgalu anbaye ni Naibu Waziri wa Nishati,
mmesema amekabidhi taa za sola katika zahanati mbalimbali, nitazifikisha kwake,
nasi tupo pamoja katika kuhakikisha tunaisaidia serikali kwenye sekta
mbalimbali," alisema Vulu.
Katika
ziara hiyo Vulu amekabidhi kitanda kimoja, shuka pamoja na vifaa Tiba katika
zahanati ya Malimbani iliyopo Kata ya Kiegeani, huku akiahidi kuchangia pesa
taslimu kwenye ujenzi wa jengo la ofisi ya Jumuia hiyo wilayani hapa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa UWT wilayani hapa Mtumwa alisema kuwa Jumuia yao
inaendelea na uhamasishaji wa Jumuia pamoja na chama ili kuhakikisha
wanaisaidia serikali katika maendeleo ya nyanja zote.
Kwa
upande wake Mjumbe wa jumuia hiyo wilayani Mafia Arafa Kisela, amemshukuru
Vulu kwa ushirikiano aliowapatia wa gari kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, huku
akiwataka wana-CCM kuendeleza umoja upendo na mshikamano.
No comments:
Post a Comment