Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano
wa Wadau uliokuwa na lengo la kupanga mikakati ya kupiga vita ugonjwa wa kifua
kikuu. Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
leo Aprili 15, 2019.
....................................
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa Dini pamoja na
wanasiasa hususani katika kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za
mitaa kuwaeleza wananchi kuwa kifua kikuu kipo lakini ukigundilika mapema
kinatibika.
Amesema kuwa nivema viongozi hao
wakawaeleza waumini wao na wapiga kura wao kujenga nidhamu ya kupima afya zao
na pindi wanapogunfulika wanakifua kikuu wawahi Hospitali mapema kwani
kinatibika.
Waziri Ummy aliyasema hayo jana
jijini Dar Es Salaam katika Uzinduzi wa ushirika wa kutokomeza kifua kikuu
nchini ambapo alisema kila mwaka watu 154,000 wanagundulika kuwa na ugonjwa wa
kifua kikuu.
” Nawaomba viongozi wangu wa Dini
kutumia siku za Jumapili na Ijumaa katika mawaidha yao kwa waumini basi
wahakikishe wanawahamasisha kupima afya zao na pindi wanapogundulika kuwa wana
ugonjwa wa kifua kikuu Mara moja wakapate tiba kwani ugonjwa huo unatibika.”
alisema.
Nakuongeza kuwa hata wanasiasa kwa
maana waheshimiwa wabunge na wenyeviti wa serikali za mitaa hususani katika
kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kuhamasisha watu wao kuangalia afya zao.”
Alisisitiza Ummy.
Waziri Ummy alisema takwimu za mwaka
2017 zinaonyesha kuwa jumla ya 443 wa kifua kikuu ni sugu waligundiliwa
na kuazishiwa matibanu na kati ya 1700 wanaokadiliwa kuwa ugonjwa
huo ambao ni sawa na 26 asilimia tu.
Pia alisema katika mwaka
2018 walikuwa wamewafikia wagonjwa 75,845 sawa na ongezeko la
asilimia 22 kutoka mwaka 2015.
Pia alizipongeza taasisi
binafsi kushirikiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa huo wa kifua
kikuu nchini nakwamba katika mapambano hayo waganga wa jadi ni watu
muhimu kwani nao wamekuwa wa athirika wakubwa katika vilinge vyao.
Aliongeza kuwa ugonjwa wa kifua kikuu
unaathari kubwa kwani katika mtu mmoja wa kifua kikuu anauwezo wa
kuambukiza watu kumi hivyo lazima mapambano dhidi ya kifua kikuu yaongezeke.
Kwaupande wake mtoa mada Kutoka
wizara ya Afya ,ambaye pia ni Meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu
na ukoma nchini, Dkt Beatrice Mutayoba alisema maeneo ya
mikusanyiko kwa ujimla wake yanaweza kupatikana maambukizi ya ugonjwa wa kifua
kikuu.
Alisema pia mapambano hayo dhidi ya
kifua kikuu si upande mmoja bali ni watu wote wanatakiwa kushirikiana na
kwa kufanya hivyo kwa pamoja ugonjwa huo unaweza Kumalizika.
Katika Uzinduzi huo pia ulihudhuliwa
na mganga Mkuu wa Serikali Profesa, Muhamed Kambi Mwakilishi Mkazi wa
shirika Afya Duniani (who ) Dkt Tigest Ketsela Mkurugenzi wa
Huduma za kinga Dkt. Leonard Subi ,Mwenyekiti wa umoja wa wabunge
wanaopambana na ugonjwa wa kifua kikuu Oscar Mkasi.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari, akitoa ufafanuzi katika katika baadhi ya mambo wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Wadau uliokuwa na lengo la kupanga mikakati ya kupiga
vita ugonjwa wa kifua kikuu. Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya New Africa
jijini Dar es salaam leo 15, 2019.
Baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano huo
uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa leo 15, 2019.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
wazee na watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
mkutano huo mara baada ya kuufumgua rasmi.
No comments:
Post a Comment