Naibu waziri wa Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba (Mb)
akiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa arusha alipokutana na wataalamu wa kilimo
,ushirika na umwagiliaji kabla ya kuanza ziara ya kuzungukia maeneo
mbalmbali mkoani hapo.
...............................
Bashiri
Salum,Wizara ya Kilimo Arusha
Vyama vya Ushirika vimeshauriwa
kukopa fedha kwenye Mabenki kwa ajili ya wanachama wao kwa kuwa
waliowengi hawakopesheki hivyo kufanya shughuli za kilimo kuwa ngumu.
Akizungumza katika kikao kilicho
wakutanisha Maafisa Ushirika, umwagiliaji na afisa kilimo Mkoani Arusha
Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari Mgumba amesema miundombinu mingi ya umwagiliaji
inahitaji marekebisho makubwa ili kuweza kutumiwa na wakulima.
Aidha miundombinu hiyo imekosa
ukarabati kutokana na wakulima kutokuwa na mitaji ya kutosha na kutoaminiwa na
taasisi za fedha kusaidia ukarabati huo.
Ameshauri tume ya Ushirika kuvisimia
vyama vya ushirika ili viweze kukopa fedha Benki Kwa ajili ya wanachama lengo
likiwa ni kufanya ukarabati Wa miundombinu ya umwagiliaji ambapo kila
mwanachama atawajibika kuchangia huduma hiyo.
Hatuwezi kufanya Kilimo cha
kibiashara Kwa kutegemea mvua ambazo Nazo zimekuwa haziyabiriki nawashauri tume
ya Ushirika na tume umwagiliaji kusimamia vyama hivyo kwenye skimu mbalimbali
za umwagiliaji kukopa fedha ambazo zitatumika kurekebisha miundombinu ya
umwagiliaji badala ya kutegemea serikali, alisema Mhe. Naibu Waziri.
Naibu Waziri aliwataka maafisa ugani
kuwafikia wakulima na kuelimisha namna ya kutumia na kutoa elimu juu ya
matumizi bora ya viuatilifu vya mimea ili kupambana na visumbufu vya mazao
ambavyo vimekuwa vikimsababishia mkulima hasara kubwa.
Naye afisa Umwagiliaji wa kanda
mhandisi Juma Mdete amesema katika ukanda huo eneo ambalo linafaa kwa kilimo
cha umwagiliaji ni hekta elfu 40 kati ya hilo linalotumika ni hekta elifu
24 tu.
Amesisitiza kwamba pamoja na matumizi
kidogo ya eneo la umwagiliaji lakini maeneo yanayomwagiliwa yanasaidia
upatikanaji wa chakula wakati wa ukame.
Akichangia wakati wa mjadala huo
Afisa Kilimo Mkoa wa Arusha Bwana Daniel Loiruck amethibitisha kwamba ukiondoa
Magonjwa ya mlipuko na uvamizi wa visumbufu vya mimea maafisa kilimo
wamekuwa wakijitahidi kuwafikia wakulima ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Naye mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akamueleza Mhe. Naibu
waziri kwamba hali ya ukame mkoani humo ni kubwa hivyo kuishauri serikali
kuanza kufikiri njia mbadala ya kupambana na hali hiyo.
‘Msimu wa kilimo upo katikati lakini mpaka sasa hakuna mvua na
tumezunguka sehemu mbalimbali hapa arusha mahindi yamekauka hata mvua ikinyesha
haiwezi kuleta mabadiliko tunaishauri serikali kufikiri mbinu za
kukabiliana na hali hiyo’. Alisisitiza bwana Loata Sanare
No comments:
Post a Comment